Featured Kitaifa

BI. NOMBO: NJOONI MPATE ELIMU KWENYE BANDA LA WIZARA

Written by mzalendo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akimsikiliza Afisa Dawati la Wanawake Wizara ya Fedha Bi. Wapheba Settembo, alipotembelea Banda la Wizara kujionea huduma zinazotolewa na Wizara wakati wa maonesho ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma.
 
Afisa Hesabu Mkuu, Kitengo cha Pensheni, Wizara ya Fedha Bi.Joyce Chacky, akitoa elimu kuhusu utaratibu wa kupokea pensheni kwa Bi.Esther Mkufya alipotembelea Banda la Wizara wakati wa maonesho ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mashujaa, Jijini Dodoma.
 
Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha Bi. Fauzia Nombo (katikati), Afisa Dawati la Wanawake Wizara ya Fedha Bi. Wapheba Settembo (kulia) na Katibu wa Wanawake Wizara ya Fedha Bi. Mariamu Kiange, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo walioshiriki katika maonesho ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma.
Baadhi ya mabanda yaliyopo katika viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma ambapo maonesho yanafanyika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Na Josephine Majura na Asia Singano WF – Dodoma
 
Wizara ya Fedha imewataka wananchi wa mkoa wa Dodoma kutembelea Banda la Wizara hiyo ili kupata elimu ya fedha, pensheni na  majukumu mbalimbali yanayofanywa na Wizara  hiyo.
 
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha Bi. Fauzia Nombo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El-maamry Mwamba, kwenye maonesho ya kuelekea kilele cha maadhimiho ya siku ya wanawake duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mashujaa, Jijini Dodoma.
 
Bi. Nombo alisema kuwa wanawake wamekua mstari wa mbele kujihusisha na masuala ya fedha ikiwemo vikoba na michezo mbalimbali yanayohusisha fedha hivyo ni vyema wakatembelea Banda hilo ili kujipatia elimu ya masuala ya mikopo na Taasisi rasmi zinazokopesha kwa riba nafuu ili kuepuka matapeli na kufirisiwa mali zao pindi watakaposhindwa kurejesha.
 
“Kuhusu elimu ya pensheni, kumekuwa na utapeli unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii hivyo ni vyema wananchi wakafika bandani hapa ili kupata uelewa wa masuala  ya pensheni ikiwemo utaratibu wa kupata pensheni zao bure bila kulipia gharama zozote”.Alisisitiza Bi. Nombo.
 
Maonesho hayo ya siku tano yamefunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.
 
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani hufanyika kila ifikapo Machi 8 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kitaifa yatafanyika Jijini Dodoma, yakiwa na kauli mbiu ya ‘’Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii, huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa.

About the author

mzalendo