Featured Kitaifa

RAIS MSTAAFU DKT KARUME NA GAVANA WA BOT WATOA MKONO WA POLE KWA RAIS WA ZANZIBARB MHE. DK.HUSSEIN MWINYI IKULU MIGOMBANI ZANZIBAR

Written by mzalendo

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kushoto kwa Rais)  wakizungumza na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Abeid Karume, alipika Ikulu Migombani kwa ajili ya kutowa mkono wa pole, kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa Kijijini kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja .(Picha na Ikulu)

RAIS Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dkt.Amani Abeid Karume akiagana na Mkewe wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, baada ya kumaliza kutowa mkono wa pole na kuhani msiba wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, Ikulu Migamoni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania  Emmanuel Tutuba, alipofika Ikulu Migombani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, kwa ajili ya kutowa mkono wa pole na kuhani, msiba wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa Kijiji kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.n 5-3-2024.Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba, alipofika Ikulu Migombani kwa ajili ya kutowa mkopo wa pole, kufuatia msiba wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa Kijijini kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu) 

About the author

mzalendo