Uncategorized

RAIS SAMIA ATOA HELIKOPTA KWA MAWAZIRI KUTAFUTA UFUMBUZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA YA LIWALE – LINDI

Written by mzalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Helikopta kwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Deo Ndejembi kufika Wilaya ya Liwale kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya miundombinu ya barabara na madaraja kutokana na mvua kubwa kunyesha na kusababisha barabara kufungwa.

Mawaziri hao wamewasili Wilayani Liwale Mkoani Lindi leo tarehe 05 Machi 2024 wakiwa wameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na Wataalam kutoka Wakala ya Barabara (TANROADS) na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya miundombinu ya barabara na madaraja yanayounganisha Wilaya hiyo na sehemu nyingine kujaa maji.

About the author

mzalendo