Kimataifa

MIILI 20 YA WAHAMIAJI YAPATIKANA KWENYE BAHARI NCHINI SENEGAL

Written by mzalendo

Gavana wa eneo hilo ameiambia AFP kuwa waokoaji wameopoa zaidi ya miili 20 kwenye bahari kaskazini mwa Senegal baada ya boti iliyokuwa inawasafirisha wahamiaji hao kuelekea Ulaya kuzama huku hofu ikiongezeka kuhusu wahamiaji waliotoweka.

“Zaidi ya miili 20 ilipatikana, gavana wa mkoa wa Saint Louis Alioune Badara Samb alisema kwa njia ya simu, akiongeza kuwa zaidi ya watu 20 waliokolewa.

Badara Samb hakusema ni abiria wangapi waliokuwa ndani ya boti hiyo lakini manusura waliiambia AFP kwamba mamia ya watu walikuwa ndani ya boti hiyo.

Mamady Dianfo, manusura kutoka eneo la Casamance kusini mwa nchi, alisema kulikuwa takriban abiria 300 wakati boti hiyo ilipoondoka Senegal wiki iliyopita.

Manusura mwingine, Alpha Balde alizungumzia abiria 200.

About the author

mzalendo