Mahakama ya Wilaya ya Bukoba Mkoa wa Kagera imemuhukumu mshitakiwa Munziru Mudrikati(19),mkulima,mkazi wa mtaa wa Nyakanyasi katika manispaa ya Bukoba kwenda jela miaka 20 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la shambulio la aibu kumchezea sehemu za siri kwa uume wake mtoto wa kike (9) mwanafunzi wa darasa la tatu.
Mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 11,2023 majira ya saa tatu na nusu asubuhi huko katika mtaa wa Nyakanyasi manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera baada ya kumrubuni madhula kuwa anaenda kumpa papai na pipi na kumuingiza chumbani kisha kuanza kumsugua na uume wake sehemu ya juu ya ukeni mwa mtoto huyo.
Akitoa hukumu hiyo Februari 27,2024 hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mheshimiwa Yona amesema kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.
Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanao jihusisha na vitendo vya ukiukaji wa sheria,maadili na ukatili dhidi ya watoto.