Featured Kitaifa

TRA SHINYANGA YAENDESHA SEMINA YA KODI KWA WATUMISHI WA TAASISI ZA UMMA SHINYANGA

Written by mzalendoeditor
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua semina ya Kodi kwa Watumishi wa taasisi za Umma mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua semina ya Kodi kwa Watumishi wa taasisi za Umma mkoa wa Shinyanga
 
Na Kadama Malunde _ Malunde 1 blog
 
Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Shinyanga imeendesha semina ya Kodi kwa Watumishi wa taasisi za Umma kwa ajili ya kukumbushana na kuelimishana kuhusu ukusanyaji wa kodi hususani matumizi na umuhimu wa kudai risiti sahihi za Kielekroniki (EFD) kwa manunuzi yote au huduma.
 
Akizungumza leo Jumatano Februari 28,2024 wakati wa kufungua semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amewataka washiriki wakawe mabalozi na walimu wazuri kwa watumishi wengine ambao hawajapata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo.
 
Mhe. Samizi amesema ni agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba TRA inakusanya kodi kwa haki na kukubaliana juu ya namna bora ya kulipa kodi bila kuathiri shughuli za kiuchumi.
 
“Kwa kutambua mchango mkubwa wa watumishi wa umma katika kuchangia pato la serikali kwa makato ya kodi ya utumishi (PAYE) yanayokatwa moja kwa moja na mwajili kila mwezi. Makusanyo haya ya kodi ya PAYE yameifanya serikali ya awamu ya sita kuweza kutekeleza miradi mingi ya maendeleo na ya kimkakati kwa kasi pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi”, amesema Mhe. Samizi.
 
Katika hatua nyingine amewapongeza watumishi wote ambao pia ni wafanyabiashara kwa kuendelea kutii sheria za kodi kwa hiari na kuendelea kulipa kodi katika biashara zao kwa kutoa risiti za EFD pale wanapofanya mauzo au kutoa huduma.
 
Aidha amewashauri watumishi wa umma kuamsha ari na mazoea ya kudai risiti sahihi za EFD kila wanapofanya manunuzi na kupokea huduma yoyote akisisitiza kuwa watumishi wana wajibu mkubwa wa kusaidia ukusanyaji wa kodi.
 
Mhe. Samizi ameitaka TRA kuchukua hatua stahiki za kudhibiti ukwepaji kodi kutokana na kutotoa risiti sahihi kwa kutoa faini stahiki kwa mujibu wa sheria.
 
“Nafahamu zipo faini zinazotolewa kwa wasiotoa na wasiodai risiti. Lengo la serikali ni kukusanya kodi si adhabu, riba na faini”, amesema.
 
Katika hatua nyingine amesema serikali itaendelea kushirikiana na TRA katika kusimamia maelekezo ya serikali kuhusu usimamizi wa mapato sambamba na suala la risiti za EFD huku akiwahimiza TRA kuendelea kufanya kazi kwa mujibu wa sheria za kodi na kwa uadilifu mkubwa.
 
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Mdessa, amesema TRA ina jukumu la kuendesha semina elekezi kwa viongozi na watumishi wa umma ili kufanikisha ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato ya serikali, kusaidia kubaini ukwepaji wa kodi, kupanua wigo wa walipakodi na uwajibikaji na kuweza kujadili utendaji na mikakati itakayosaidia kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.
 
Mdessa amesema suala la kodi ni mtambuka kwa ajili ya maendeleo ya taifa hivyo kuwasisitiza wafanyabiashara kutoa risiti na wateja kudai risiti.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua semina ya Kodi kwa Watumishi wa taasisi za Umma mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua semina ya Kodi kwa Watumishi wa taasisi za Umma mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Mdessa akizungumza wakati wa semina ya Kodi kwa Watumishi wa taasisi za Umma mkoa wa Shinyanga

About the author

mzalendoeditor