Featured Michezo

OFISI YA WAZIRI MKUU YASHIRIKI KILI MARATHON

Written by mzalendoeditor

Na: Mwandishi Wetu – Kilimanjaro

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na OSHA imeshiriki mashindano ya Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro (Kilimanjaro International Marathon 2024) Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Februari 25, 2024

Aidha, Katika mbio hizo, wanariadha hao wameshiriki mbio za Kilometa tano (Fun run) na wengine wameshiriki mbio za umbali wa kilometa 21 (Tigo half Marathon).

Akizungumza mara baaada ya kushiriki mbio hizo, Mkurugenzi wa Msaidizi wa Utawala, Edith Semtengu amesema Ofisi hiyo imekuwa ikishiriki katika Mashindano hayo kwa lengo la kutangaza majukumu ya ofisi hiyo katika mbio hizo sambamba na kuimarisha afya za watumishi.

Vile vile, Mkurugenzi huyo amewasihi wafanyakazi kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi ili kulinda afya zao.

Katika Mashindano hayo, Ofisi hiyo ilishiriki pamoja na Taasisi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA).

About the author

mzalendoeditor