Kimataifa

RAIS WA ZAMANI WA TUNISIA JELA MIAKA NANE

Written by mzalendo

Vyombo vya habari vya ndani nchiniTunisia vimeripoti kuwa Rais wa zamani wa hiyo Moncef Marzouki na mkosoaji mkali wa mkuu wa sasa wa nchi hiyo Kais Saied, amehukumiwa bila kuwepo kifungo cha miaka minane jela kwa kujaribu “kuchochea machafuko” nchini humo.

Vimesema uamuzi hu0 ulitamkwa na chumba cha jinai cha Mahakama ya Mwanzo ya Tunis akiwa anaishi nchini Ufaransa, Bw. Marzouki, rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Tunisia baada ya mapinduzi ya mwaka 2011, anashitakiwa katika kesi hii baada ya taarifa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Alipatikana na hatia katika tukio la kwanza la kujaribu “kubadilisha muundo wa serikali”, “kuwachochea watu kujizatiti dhidi ya kila mmoja wao” na “kusababisha machafuko na uporaji” nchini, imeripoti redio ya kibinafsi ya Mosaïque FM ikinukuu chanzo cha mahakama. Alipohojiwa na shirika la habari la AFP, msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Tunis hakuweza kupatikana.

Mwishoni mwa mwaka 2021, Bw. Marzouki alikuwa tayari amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa “kuhatarisha usalama wa taifa nje ya nchi” baada, wakati wa maandamano huko Paris, kuitolea wito serikali ya Ufaransa “kukataa kutoa msaada wowote” kwa Rais Saied, ambaye alishutumu kwa “kupanga njama dhidi ya Mapinduzi”.

Tangu mwezi wa Novemba 2021, amekuwa pia chini ya hati ya kimataifa ya kukamatwa iliyotolewa na jaji wa Tunisia muda mfupi baada ya Bw. Saied kuomba  kuchunguza maoni mbalimbali yaliyotolewa na Bw. Marzouki, anayetajwa kuwa “adui wa Tunisia” na kunyang’anywa hati yake ya kusafiria ya kidiplomasia. Baada ya mapinduzi ya Rais Saied mnamo mwezi Julai 2021 ambapo alijipa mamlaka yote, Bw. Marzouki aliongeza wito wake kwenye vituo vya televisheni na mitandao ya kijamii kutaka atimulimuliwe mamlakani mtu aliyemtaja kama “kiongozi wa mapinduzi” na “dikteta”.

Moncef Marzouki, mwenye umri wa miaka 79, mpinzani wa kihistoria wa udikteta wa Ben Ali wakati huo aliyekuwa rais wa kwanza wa baada ya mapinduzi (2011-2014), kwa muda mrefu alitangaza kupigania demokrasia nchini Tunisia, hata kama taswira yake imefifia kutokana na uhusiano wake wenye utata na chama cha kihafidhina cha Kiislamu cha Ennahdha, kutokana na kwamba alishinda uchaguzi wa rais, kulingana na wachambuzi.

About the author

mzalendo