Featured Kitaifa

RAIS DKT.MWINYI ATETA NA BALOZI WA UINGEREZA, UJUMBE WA KAMPUNI YA NUTRI-SAN

Written by mzalendo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. David Concar, wakibadilishana mawazo baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao na Ujumbe wa Kampuni ya Nutri-San Ltd ya Uingereza, yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nutri-San ya Uingereza inayojenga Kiwanda cha Mwani Chamanangwe Pemba na (kulia kwa Rais) Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. David Concar na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeeo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaban, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe.David Concar (kulia kwa Rais ) akiwa na Ujumbe wa Kampuni ya Nutri –San Limited ya Uingereza inayojenga Kiwanda cha Mwani Chamanangwe Pemba, ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nutri – San Ltd. San Chau (kulia kwake) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaban.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendo