Featured Kitaifa

KAMATI YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA YARIDHISHWA NA MAENDELEO KIWANDA CHA STAMICO.

Written by mzalendoeditor

Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma imeridhishwa na maendeleo ya kiwanda kilichopo chini ya Stamico walipotembelea Leo tarehe 20 Februari 2024 Jijini Mwanza

Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Deus Clement Sangu alihitimisha Kikao baada ya ukaguzi wa kiwanda cha Mwanza Precious Metals Refinery Mwanza akisema

“Uwekezaji umekuwa kwenye Kampuni ya Stamico na ni shirika la kuigwa na itaenda kuipeleka mbali sekta hii ya madini “

Mwenyekiti aliwahakikishia Stamico kwamba kamati itawasaidia kwa vile vinavyowakwaza ili waendelee kufanya vizuri na kukuza pato la Taifa.

About the author

mzalendoeditor