Featured Kitaifa

WAZIRI SILAA AKABIDHI MAGARI YENYE THAMANI YA BIL.2.07 MRADI WA LTIP

Written by mzalendo
WAZIRI  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa akiwasha gari kuashiria kuanza kwa matumizi ya gari mpya kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Jerry Slaa, amekabidhi magari 16 yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 2.079 yatakayosaidia kupunguza gharama za kukodi magari wakati wa utekelezaji Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP).
Akizungumza katika hafla hiyo ya  iliyofanyika leo Februari 19,2024 katika  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodom,Waziri  Slaa,amesema kuwa magari hayo yatasaidia kutekeleza  mradi  huo katika sekta ya ardhi.
Waziri Slaa amesema kuwa  magari hayo 16 yatakwenda kusaidia kuharakisha utekelezaji wa mradi huo ambao umejikita katika kuboresha milki za ardhi mijini na vijijini.
“Mradi huu utakwenda kuwa suluhu kubwa katika sekta ya ardhi kwani utasaidia kupima pamoja na kupanga matumizi bora ya ardhi mijini na vijijini na kutoa hati miliki kwa wananchi”amesema Waziri Slaa 
Aidha Waziri Slaa,amemuagiza mratibu wa mradi huo kuhakikisha kuwa magari hayo yanatumika kwa matumizi yaliyopangwa na sivyo vinginevyo.
‘’Magari haya yatumike kwa kazi za mradi wale wote watakao kabidhiwa magari haya wayatumie vizuri, wayatunze tusione magari haya yamebeba mkaa  au kufanyika katika shughuli za harusi tungependa kuyaona yakifanya kazi ya Mradi ili mradi ukiisha tuyatumie katika wizara yetu kwenye majukumu mengine’’. amesisitiza 
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga  amesema thamani ya gari moja ni takribani Mil. 129.9 za Tanzania na magari hayo ni sehemu ya magari 70 yatakayonunuliwa kwa msaada wa Benki ya Dunia.
“Magari haya 16 ambayo Mweshimiwa Waziri unakabidhi ya mradi huu ni sehemu ya mengine 59 ambayo yataingia bandarini na bei ya kila gari ni Sh.milioni 129.9 na bei imeshuka kutoka na kununua kwa kutumia wakala Benki ya Dunia na mara baada ya kukabidhiwa leo hii hapa yatakwenda katika maeneo yanakohitajika”amesema Mhandisi Sanga
Mhandisi Sanga amesema kuwa Mradi huo  wa uboreshani wa milki za ardhi utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano utaogharimu zaidi ya Sh.bilioni 346 ikiwa ni mkopo kutoka benki ya Dunia  (WB).
Naye  Mratibu  wa Mradi wa LTIP  Bw. Joseph I.Shewiyo  amesema  magari  hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa utekezaji wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu kuu nnne ambazo ni Usalama wa Milki, uimarishaji mifumo ya taarifa za Ardhi na ujenzi wa miundombinu ya Ardhi.
“Kupitia mradi huu  kila mmoja atakua na hati yake na hati miliki inatolewa bure mwaka huu tumepanga kufikia vijiji 700 hadi sasa tayari tumefikia vijiji  540.Pia tumepanga kufika katika mitaa 660 na halmashauri 36, lakinj pia mradi huu hadi sasa umetoa ajira kwa watu zaidi ya 700″amesema Bw.Shewiyo
 
WAZIRI  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa  akikata utepe kukabidhi magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa akiwasha gari kuashiria kuanza kwa matumizi ya gari mpya kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
 
WAZIRI  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa ,akimkabidhi ufunguo wa gari Katibu Mkuu Wizara  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi. Anthony Sanga kwa ajili ya kumkabidhi  Mratibu wa Mradi huo.
 Katibu Mkuu Wizara  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akikabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Mradi huo Bw. Joseph Shewiyo  kama ishara ya kuanza kutumika kwa magari hayo kwenye Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa,akizungumza mara baada ya kukabidhi  magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
KATIBU  Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi  magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
 
Mratibu  Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) Bw. Joseph I.Shewiyo ,akielezea jinsi magari yatakavyotumika wakati wa hafla ya kukabidhi  magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi
  hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
 
MUONEKANO wa Magari 16 yaliyokabidhiwa na Waziri  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.

About the author

mzalendo