Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowasa Kijijini Ngarash Wilayani Monduli leo Februari 16, 2024.
Sekta ya Afya itaendelea kumuenzi Hayati Edward Lowasa kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika maendeleo ya Sekta ya Afya kwa kushiriki kikamilifu kwenye uhuishaji wa Sera ya Afya ya Mwaka 2007, ambayo inatoa dira katika upatikanaji wa huduma za matibabu nchini.
Hayati Lowasa aliongoza katika uandaaji wa Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi ambao ulituongoza katika kuibua miradi ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya hadi ngazi ya msingi ya jamii na sasa tunashuhudia matunda ya kuwa na Vituo hivyo hadi ngazi ya Jamii (Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za Wilaya)
“Natoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Watanzania wote kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowasa. Kifo chake kimetugusa wengi, tutaendelea kummuenzi kwa mema yote aliyotufanyia lakini kikubwa zaidi kuziishi falfasa zake za utumishi uliobora katika kuwatumikia Wananchi” amesema Dkt. Mollel.
Buriani Hayati Edward Lowasa.