Kimataifa

BURKINA FASO, MALI NA NIGER KUUNDA SHIRIKISHO

Written by mzalendo

Mawaziri wa Burkina Faso, Mali na Niger wamekutana katika mji mkuu wa Burkina Faso kujadili kuunda shirikisho.

Serikali hizo tatu za kijeshi mwezi Septemba ziliunda mkataba wa ulinzi na uchumi, muungano wa nchi za Sahel (AES).

Waziri wa ulinzi wa Burkina Faso Jenerali Kassoum Coulibaly amesema mazungumzo ya Ouagadougou yalikuwa fursa ya kuendelea kutekeleza mikataba, mikakati na taratibu na muundo wa kisheria kwa ajili ya shirikisho.

Taratibu hizo” zitaruhusu muungano wetu na shirikisho kufanya kazi kwa ufanisi na kwa furaha kubwa” ya wanainchi wa nchi hizi tatu, mwenzake wa Niger Jenerali Salifou Modi amesema.

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa hayo matatu wanaunga mkono uundaji wa shirikisho kama sehemu ya lengo la muda mrefu la kuziunga nchi hizo jirani za Afrika Magharibi ndani ya shirikisho, kwenye mkutano wa mwezi Disemba katika mji mkuu wa Mali wa Bamako.

About the author

mzalendo