Featured Kitaifa

NIDA YAZINDUA UGAWAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA SHINYANGA

Written by mzalendoeditor
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Shinyanga, imezindua rasmi zoezi la ugawaji wa Vitambulisho hivyo kwa wananchi.
Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 15, 2024 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, na kuzinduliwa Rasmi na Mkuu wa Mkoa huo Christina Mndeme na kisha kuwakabidhi Vitambulisho vya Taifa Wakuu wa wilaya ili vikasambazwe kwa wananchi.
Afisa Msajili wa NIDA Mkoa wa Shinyanga Nathanael Njau akizungumza kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa, amesema Mamlaka hiyo imeandaa mpango kazi wa ugawaji wa Vitambulisho hivyo kwa Wananchi pamoja na kuendelea kufanya usajili.
“Zoezi hili la ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea tunaomba kupata ushirikiano wako Mkuu wa Mkoa na timu yako katika usafiri na ushauri, ili kuhakikisha uhamasishaji wa zoezi hili unafanyika katika ngazi zote ili wananchi waweze kuitikia wito na wachukue Vitambulisho katika maeneo yao,”amesema Njau.
Aidha, amesema katika Mkoa huo wa Shinyanga wameweza kusajili jumla ya wananchi 718,243 kati ya 833,279 ya waliokusudiwa kusajili sawa na asilimia 86 ya usajili.
Pia ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia namna ambavyo imeendelea kuipa nguvu Mamlaka hiyo katika kutimiza majukumu yake, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kushirikiana nao.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ametoa Maagizo kwa Wakuu wa wilaya mkoani humo mara baada ya kuwakabidhi Vitambulisho hivyo, kwamba wavisimamie na kuwafikia walengwa.
Amewataka pia wananchi ambao bado hawajajisajili ili kupata Vitambulisho vya Taifa, kwamba wakajisajili sababu Vitambulisho hivyo ni haki ya kila Mtanzania.
 
“Tunataka kila Mtu awe na Kitambulisho cha Taifa badala ya kuwa na Namba ya NIDA, nendeni Mkajisajili na Vitambulisho hivi vitawafikia popote mlipo Mheshimiwa Rais hataki wananchi wake wapate usumbufu bali mtaletewa kwenye maeneo yenu,”amesema Mndeme.
Aidha, amewataka pia wananchi wale ambao wamshapoteza Vitambulisho vyao, kwamba wafikie kwenye Ofisi za Msajili ili wapate Vitambulisho vingine.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye zoezi la uzinduzi wa ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi.
Afisa Msajili wa NIDA Mkoa wa Shinyanga Nathanael Njau akizungmzia uzinduzi wa zoezi la ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi.
Afisa Msajili wa NIDA Mkoa wa Shinyanga Nathanael Njau akizungmzia uzinduzi wa zoezi la ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wnaanchi.
Afisa Msajili wa NIDA Mkoa wa Shinyanga Nathanael Njau, (kushoto) akimpatia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, Vitambulisho vya Taifa kwa ajili ya kuwapatia Wakuu wa wilaya mkoani humo ili vikasambazwe kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) akimpatia Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude Vitambulisho vya Taifa ambavyo watakwenda kupewa wananchi wa wilaya hiyo waliojisajili NIDA.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) akimpatia Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude Vitambulisho vya Taifa kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi ambavyo watakwenda kupewa wananchi wa wilaya hiyo waliojisajili NIDA.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) akimpatia Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita Vitambulisho vya Taifa ambavyo watakwenda kupewa wananchi wa wilaya hiyo waliojisajili NIDA.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo wa ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa Wananchi.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.

About the author

mzalendoeditor