Kitaifa

RAIS SAMIA KATIMIZA MAJUKUMU YAKE, SASA JUKUMU LINABAKI KWENU – WAZIRI UMMY

Written by mzalendo


Na Gideon Gregory, Dodoma.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwisha kutimiza majukumu yake katika sekta ya afya hivyo ni jukukumu la waganga Wafawidhi kwenda kutimiza majukumu yao.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Februari 14,2024 Jijini Dodoma wakati akifunga mkutano wa mwaka wa Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya Msingi na kuongeza kuwa kadri huduma zinavyozidi kupanuliwa katika maeneo yote nchini ndivyo wahitaji wanazidi kuongezeka.

“Nataka niwashukuru sana kwani mnafanya vizuri katika maeneo yenu licha ya changamoto mbalimbali mnazozipitia ndiyo maana kila siku naendelea kuwa mtetezi wenu, unakuta ninyi mmekuja hapa lakini kuna kituo kimefungwa mtoa huduma wao kaja hapa kwakweli niwapongeze sana kwa namna mnavyojitoa,”amesema.

Waziri Ummy amesema kuwa kwasasa hawatokagua suala la huduma tu wanazozitoa wataingia mpaka kwenye upande wa vipimo vya maabara ili kuweza kusaidia utoaji wa huduma bora unaendelea kuimarika.

Aidha amewataka waganga wafawidhi hao kuhakikisha huduma zinazotolewa katika vituo vya afya zinazigatia ustawi wa jamii kwa kuanzisha dirisha la kuhudumia wazee pamoja na kuweka takwimu za wagonjwa wanaotumia huduma za msamaha zinarekodiwa.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Wilson Mahera amemuomba Waziri Ummy mwongozo wa uchangiaji wa bima za afya ukamilike kwa wakati ili kuwasaidia watumiaji wa huduma hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Rashidi Mfaume amesema kuwa waliamua kufanya mkutano huo kwasababu kumekuwa na nafasi kubwa ya mawasiliano na kushindwa kupata marejesho wa kiutendaji kutoka kwao baadala yake kupata kutoka kwa vyombo vya habari na wananchi.

“Tumekuwa na uwekezaji mkubwa kuanzia ngazi ya msingi kwenye upande wa dawa na vifaa tiba na sasa Rais hatumdai bali yeye anatudai na ni fursa kwao waganga hawa kubadiliashana uzoefu katika utendaji wao wa kazi,”amesema.

Amesema kuwa moja kati ya malengo makubwa ya mkutano huo ni kuwajengeana uwezo katika nafasi mbalimbali za utendaji kazi ikiwemo kupata taarifa kuhusiana na afua mbalimbali zinazoendeshwa na na Serikali na hali ya ufuatiliaji utendaji wa kazi unaofanywa na TAMISEMI.

“Pia kupitia mkusanyiko huu tumepata maoni mbalimbali na tunaahidi kwenda kuyafanyia kazi maoni yao ambayo wameyawasilisha ndani ya siku hizi mbili tulizokutana nao hapa.

Akisoma risala kuhusiana na hali ya utendaji kazi mbele ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Mwenyekiti wa Waganga Wafawidhi Dkt. Florence Hilar ameipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini ikiwemo kununua vifaa tiba, ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo ya karibu na wananchi.

Serikali imeendelea kufunga mifumo ya kielektroki katika vituo mbalimbali vya afya jambo ambalo limelekea kukabiliana na upotevu wa fedha uliokuwepo hapo awali na hiyo kusaidia ongezeko la ukusanyaji wa mapato kupitia sekta ya afya.

“Tunaipongeza Serikali kwa kuendelea kusimamia vyema sera ya afya ya mwaka 2007 na kutekeleza vyema irani ya chama katika kuendelea kuboresha huduma za afya nchini,”amesema.

Pia ameongeza kuwa lengo la uanzishwaji wa maduka ya madawa ni kurahisisha upatikanaji wa dawa kwa urahisi kwa wagonjwa lakini changamoto inakuwa ni pale ambapo mgonjwa anayetibiwa kwa msamaha akitakiwa kulipia dawa hizo.

Amesema upatikanaji hafifu wa dawa kutoka bohari kuu ya dawa kunaathiri hali ya utoaji wa huduma kwa kwa wananchi.

About the author

mzalendo