Featured Kitaifa

700 KUFANYIWA UCHUNGUZI WA MOYO BMH

Written by mzalendoeditor

Watu 700 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa moyo kwenye kambi ya moyo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).

Daktari Bingwa Moyo wa BMH, Dkt Calvin Masava, amesema leo kuwa BMH inashirikiana na madaktari sita kutoka Netherlands kufanya kambi hiyo ya moyo.

“Lengo la kambi mbali na kutoa huduma lakini inalenga kubadilishana uzoefu na wenzetu kutoka Netherlands,” anasema Daktari huyo bingwa wa moyo.

Dkt Masava amefafanua kuwa watakaokutwa na matatizo ya moyo watapatiwa matibabu hapa hapa BMH.

“Hii ni kambi yetu ya kwanza ya pamoja na wenzetu kutoka nje kwa kwa mwaka huu,” ameongeza.

About the author

mzalendoeditor