Kitaifa

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKA LA KIMATAIFA (NI)

Written by mzalendo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Kimataifa la Nutrition International (NI) kutoka Canada Bw. Joel Spicer akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe.

Katika mazungumzo hayo mambo mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo; maeneo ya mashirikiano katika kupambana na lishe duni nchini.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 07 Februari, 2024 Bungeni Jijini Dodoma.

About the author

mzalendo