Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2023, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2024.

Na.Mwandishi Wetu-DODOMA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeshauri Serikali iongeze bajeti ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kufikia malengo na tija iliyokusudiwa ya kuwainua vijana kiuchumi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq (Mb) ametoa ushauri huo leo Februari 7, 2024 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2023.

Amesema kuwa, ufinyu wa bajeti
umepelekea mfuko huo kushindwa kukidhi mahitaji ya utoaji mikopo kwa vijana.

Pia, Kamati imeshauri Serikali kuunganisha mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kuwa na tija endelevu ya kuwezesha vijana kimitaji.

Previous articleKATAMBI: MAFUNZO YA PROGRAMU YA TAIFA YA KUKUZA UJUZI KUFANYIWA TATHMINI 2024/2025
Next articleMAHUNDI: “MRADI WA MAJI TUKUYU KUHUDUMIA WAKAZI ELFU 63,647

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here