Uncategorized

MRADI WA DMDP KUUNGANISHA WILAYA ZA TEMEKE NA MKURANGA

Written by mzalendo

KATIKA jitihada za kuendelea kuwaunganisha Wananchi wa Wilaya mbili za Temeke na Mkuranga, Serikali imepanga kuboresha kwa kujenga madaraja/makalavati ya Churwi, Tabowa na Majimatitu kupitia mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbagala, Mhe Abdallah Chaurembo aliyehoji mpango wa Serikali katika kuziunganisha Mbagala na Mkuranga..

“ Malengo ya Serikali ni kuziunganisha Wilaya za Temeke na Mkurang, mpaka sasa maeneo matatu ya Kilwa, Tambani na Rufu Nampombo yameunganishwa kwa madaraja/makalavati na yanapitika kwa mwaka mzima. Kwa sasa serikali imepanga kuboresha kwa kujenga madaraja/makalavati ya Churwi, Tabowa na Majimatitu kupitia mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP).

About the author

mzalendo