NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Dkt Festo Dugange amesema Serikali imezielekeza Halmashauri zote nchini kutenga bajeti na kununua mafuta kinga ya watu wenye ualbino na kuyagawa kwa wahitaji.
Mhe Dkt Dugange ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali ya Waheshimiwa Wabunge ikiwa leo ni kikao cha tano cha mkutano wa 14 wa Bunge la 12.
“ Serikali inatambua umuhimu wa kuwezesha upatikanaji wa mafuta kwa watu wenye Ualbino kupitia Halmashauri kote nchini. Katika mwaka wa fedha wa 2021/22 na 2022/23 jumla ya halmashauri 41 zilitenga na kununua mafuta kinga yenye thamani ya Sh Milioni 47 na kuyagawa kwa wahitaji,” Amesema Mhe Dkt Dugange.