Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussei Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Mhe.Zhang Zhisheng, wakati alipofika kumuaga Rais, Ikulu Jijini Zanzibar leo akiwa amemaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussei Ali Mwinyi (katikati) akizungumza na Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Mhe.Zhang Zhisheng (wa pili kushoto) alipofika kuaga Ikulu Jijini Zanzibar leo akimaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussei Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Mhe.Zhang Zhisheng, wakati wa mazungumzo yao leo alipofika kumuaga Ikulu Jijini Zanzibar akimaliza muda wake wa kazi .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussei Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Mhe.Zhang Zhisheng, leo alipofika kuaga Ikulu Jijini Zanzibar akimaliza muda wake wa kazi .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussei Ali Mwinyi (kulia) akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Mhe.Zhang Zhisheng, baada ya mazungumzo yao leo alipofika kuaga Ikulu Jijini Zanzibar akimaliza muda wake wa kazi .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussei Ali Mwinyi (kulia) akiwa katika picha na Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Mhe.Zhang Zhisheng baada ya mazungumzo yao leo alipofika kuaga Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi mdogo wa China Mhe. Zhang Zhisheng anayefanyia kazi zake Zanzibar, kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi nchini tarehe :29 Januari 2024, Ikulu Zanzibar.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Balozi Mhe.Zhang Zhisheng kwa kudumisha na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Zanzibar na China katika miaka mitatu ya utumishi wake nchini, pia kwa kuratibu vema ziara yake mwaka jana China.
Vilevile Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa China imeendelea kusaidia Zanzibar na kushirikiana katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya kwa kuleta madaktari kutoka China, ufadhili wa masomo, kujengea uwezo, biashara, utalii, pamoja na kuwepo kwa kampuni za kichina katika kazi za miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara, bandari, na uwanja wa ndege.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amewakaribisha wawekezaji kutoka China kwenye sekta ya utalii kujenga hoteli kwa kuongeza watalii zaidi wa Kichina kuitembelea Zanzibar.
Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kushirikiana na kudumisha uhusiano na China ambayo yametimiza miaka 60.
Naye Balozi Mhe.Zhang Zhisheng amesema China itaendelea kushirikiana na Zanzibar kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.