Kitaifa

BAADA YA KUWEKEWA PUTO APUNGUA KILO KUTOKA 150 HADI 99

Written by mzalendo


Bw. Vicent Fortunatus amesema huduma aliyowekewa ya puto maalumu (intragastric balloon) pamoja na kupunguza zaidi ya kilo 50 imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuondokana na changamoto ya maumivu ya mgongo, mwili kuwa mwepesi na kuwa rahisi kwake kutekeleza majukumu ambayo awali ilikuwa ngumu kuyatekeleza.

Bw. Fortunatus ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi katika kipindi cha AFYA PODCAST ambapo amebainisha kuwa hakuchanwa popote ili kuwekewa puto na ulaji wake umebadilika sana.

Aidha, Prof. Janabi ameihakikishia jamii kuwa huduma hiyo ni salama na inatumia teknolojia ya hali ya juu duniani ambapo dhumuni lake ni kumtengenezea mtu utamaduni wa kula kidogo na kwa kuzingatia mlo kamili kwakuwa puto linakuwa limechukua moja ya tatu ya tumbo na mbili ya tatu inabaki kwa ajili ya chakula.

About the author

mzalendo