Featured Kitaifa

WAZIRI NAPE AITAKA BODI YA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI KUSIMAMIA MAJUKUMU KWA KUZINGATIA SHERIA

Written by mzalendo

WAZIRI  wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,akizungumza wakati akizindua  Bodi ya Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.

KATIBU  Mkuu Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Mohamed Khamis Abdullah,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Bodi ya Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ulinzi wa Tume ya Taarifa Binafsi Balozi Adadi Mohamed Rajabu,akieleza malengo ya tume hiyo wakati wa uzinduzi wa  Bodi ya Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi ,ACP Emmanuel Mkilia,akitoa taarifa na mikakati ya tume hiyo  wakati wa uzinduzi wa  Bodi ya Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.

SEHEMU ya wajumbe wakimsikiliza Waziri   wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,(hayupo pichani)  wakati akizindua  Bodi ya Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye, akizindua  Bodi ya Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ulinzi wa Tume ya Taarifa Binafsi Balozi Adadi Mohamed Rajabu.Kushoto ni Katibu   Mkuu Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Mohamed Khamis Abdullah,

WAZIRI  wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,akikabidhi Vyeti kwa wajumbe wa  Bodi ya Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua  Bodi ya Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi hafla iliyofanyika leo Januari 19,2024 jijini Dodoma.

Na.Bolgas Odilo-DODOMA

WAZIRI  wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,ameitka Bodi ya Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi kusimamia majukumu ya Tume hiyo, kwa kuzingatia sheria katika kuhakikisha inalinda ,haki na utu wa watu wa taarifa  ili kujenga imani  kwa  watu wote  hasa wanaotoka nje  ili waone Tanzania ni sehemu salama.

Waziri Nnauye ametoa rai hiyo  leo Januari 19,2024 jijini Dodoma na  mara baada ya kuzindua  Bodi hiyo ambapo ameitaka Bodi hiyo kuanza kutoa elimu kwa umma kuhusu ulinzi wa Taarifa binafsi kupitia makongamano mbalimbali ili wawe na uelewa.

Waziri Nnauye mesema tume hiyo mpya inajukumu la kulinda heshima, haki na utu kwa kuhakikisha taarifa za watanzania na hata wageni taarifa zao kuwa sehemu salama na zinatumika kwa kujali haki heshima na utu ili watu waone Tanzania ni taifa salama kwa huduma za kidigitali
 “Wito wangu kwenu ni kuilinda imani ya Rais wetu kwani mchakato ulikuwa mkubwa kuwapata nyinyi na kuipata tume hii na ukweli kutoka moyoni ninatamani kuja kusikia tume hii ya taarifa binafsi nchini ni Bora kuliko tume nyingine duniani, ” Amesema Mhe. Nnauye
Aidha amesisitiza kuwa matumaini ya taifa ni kuona  faragha zao zinalindwa nchini kwani kuanzia sasa taarifa za watu zinakusanywa ,zinachakatwa na kutuma sehemu sahihi ambapo misingi mikuu inazingatiwa ya kikanda na kimataifa .
“Imani yangu ni  baada ya muda watu watakuja kujifunza kwetu juu ya tume hii kwani nchi ya Tanzania ni mwanachama kwa nchi mbalimbali imeanza vizuri hivyo tume kuhakikisha inaanza utekelezaji wa majukumu yake kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu zilizowekwa na msikubali kuingiliwa na badala yake mlindwe na sheria msiendeshwe, ” amefafanua
Hata hivyo ameongeza kuwa utoaji wa huduma  unaendana na huduma za kidigitali  pia mifumo isomane na iwepo  kila mkoa ili watu watumie mifumo kuliko watu kutoka mikoani kuja Dodoma au Dar es Salaam kutafuta mifumo nasisitiza muweke mifumo inayisomana.

 Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Mohamed Khamis Abdullah amesema kuwa alikuwepo wakati wa ugawaji wa vitendea kazi na mkakati huo ulikuwa unalenga mikakati mitano.

 “Hayo ni Matokeo ya siku 100 ambapo wamefanikiwa kwa asilimia 90 kwani wameweza kujenga taasisi yenye sura nzuri inaonekana kujenga utambulisho anuani pamoja na logo na wako kwenye kutengeneza mpango mkakati.”amesema Mhe.Abdullah
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ulinzi wa Tume ya Taarifa Binafsi Balozi Adadi Mohamed Rajabu,amesema kuwa  watahakikisha wanafanya kazi kwa bidii na weledi ili kuhakikisha wanalinda taarifa binafsi  kwa kuzingatia sheria.

Awali,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume  ya ulinzi wa Taarifa binafsi ,ACP Emmanuel Mkilia  amesema wamekuwa na mpango mkakati wa siku mia moja ikiwemo kujenga uelewa katika ukusanyaji Taarifa kwa taasisi ambapo wameweza kufanikiwa.

About the author

mzalendo