Featured Kitaifa

YAH: UTEUZI WA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU MZUMBE 

Written by mzalendo

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa Mamlaka  aliyonayo chini ya Kifungu cha 12 (1) cha Hati Idhini ya Chuo Kikuu  Mzumbe ya Mwaka 2007 kikisomwa sambamba na Kanuni ya 5 (1) ya  Jedwali la kwanza la Hati Idhini ya Chuo Kikuu Mzumbe ya mwaka  2007, amemteua Prof. William Senkondo Mwegoha kuwa Makamu  Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kipindi cha Miaka mitano (5) kuanzia  tarehe 8 Januari, 2024. 

Kabla ya uteuzi huu Prof. William Senkondo Mwegoha alikuwa akikaimu  nafasi hiyo. 

Tunampongeza na kumtakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu  yake. 

Imetolewa na 

Lulu Phillip Mussa 

KAIMU MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO NA MASOKO 

About the author

mzalendo