Featured Kitaifa

HOSPITALI ZA RUFAA NCHINI ZATAKIWA KUWA NA MFUMO RASMI WANANCHI KUTOA MAONI YAO

Written by mzalendoeditor

Na. Majid Abdulkarim , Tumbi- Pwani

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amesisitiza Hospitali zote za Rufaa nchini kuhakikisha zinakuwa na mfumo rasmi ambao unajulikana kwa wanachi wanaowahudumia ili kutoa mrejesho wa Huduma wanazotoa

Dkt. Jingu amebainisha hayo wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani -Tumbi, kwa lengo la kujionea hali ya utoaji wa huduma Huduma za afya katika hospitali hiyo.

Dkt. Jingu amesema njia pekee ya kuhakikisha wanaboresha Huduma kwa wananchi wanaowahudumia ni kupata mrejesho kutoka kwa wananchi wanao wahudumia.

“Tukiimarisha njia za kupata mrejesho kutoka kwa wananchi tunaowahudumia itasaidia kujua ubora wa Huduma tunaotoa upo kiasi gani kwani jukumu la hospitali za Rufaa ni kutoa Huduma kwa viwango vya juu”, ameieleza Dkt. Jingu

Dkt. Jingo ametolea mfano kuwa baadhi ya Hospiatli zimeaanza kutekeleza Mfumo huo kwa kuwa na watu maalumu wakiwa wamevaa nguo zenye maneno niulize mimi au kuwa na vituo vya huduma kwa wateja vilivyopo kusikiliza maoni, kero na pongezi za wananchi wanaowahudumia.

Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshafanya uwekezaji wa kutosha katika sekta ya afya hivyo ni jukumu la wataalamu wa afya kuhakikisha wanatoa Huduma bora kwa wananchi ili kunufaika na uwekezaji huo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumain Nagu ametoa wito kwa wataalamu wa afya kufanya kazi kwa kuzingatia Miiko na maadili ya kazi zao ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia Watanzania.

“Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuwahudumia wananchi na niwakumbushe kuwa tumekuwa na magonjwa mbalimbali ya mlipuko hivyo hakikisheni mnafanya utambuzi wa haraka kwa makini kila mgonjwa anapofika hospitali kupatiwa Huduma za a”, amesema Prof. Nagu

About the author

mzalendoeditor