Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewasili Kampala nchini Uganda ambapo anatarajia kushiriki Mkutano wa 27 wa Maspika na Makatibu wa Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola unaofanyika nchini humo kuanzia leo.

Mkutano huu unatarajiwa kuangazia na kutoa fursa kwa Viongozi wa Mihimili kupeana uzoefu na mbinu chanya mpya juu ya hatua mbalimbali za uendeshaji wa Mabunge pamoja na kujenga mahusiano mazuri zaidi yatakayoleta hamasa kwenye kufikia diplomasia ya Kibunge ndani ya Jumuiya hiyo.

Previous articleUWEKEZAJI MAHIRI KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI YA TAWA KUIINGIZIA SERIKALI ZAIDI YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 314
Next articlePATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JANUARI 4,2024

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here