Na Abel Paul,Jeshi la Polisi- Mbeya.

Jeshi la Polisi limesema mtuhumiwa Lucas Tarimio aliyekamatwa disemba 31,2023 kwa tuhuma za kumchoma visu na kusababisha kifo Beatrice Minja leo Januari 02,2024 amefariki dunia huko wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Akitoa taarifa hiyo leo Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msadizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesama kuwa mtuhumiwa huyo amefariki dunia huko Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kunywa sumu ya kuuwa wadudu wakati alipohisi kufikiwa na Mkono wa sheria.

Msemaji wa Jeshi hilo ameongeza kuwa taratibu nyingine za kisheria zinafuata kuhusiana na tukio hilo.

Previous articleBARRICK BULYANHULU YAPELEKA FARAJA YA SIKUKUU YA MWAKA MPYA KWA WAZAZI,WAGONJWA NA WATUMISHI KITUO CHA AFYA BUGARAMA
Next articleWATUHUMIWA SITA WA UVUNJAJI MIKONONI MWA JESHI LA POLISI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here