Kitaifa

ASKOFU KASSALA: SIPO TAYARI KUBARIKI NDOA ZA JINSIA MOJA, BORA NIBARIKI JIWE

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Geita.

Askofu wa Jimbo Katoliki Geita, Flavian Kassala amesema hayuko tayari kubariki ndoa zilizo kinyume na maadili kwani ni kinyume na maagano ya Mungu ya kutaka binadamu wakazaliane na kuendeleza vizazi ulimwenguni.

Askofu Kassala amesema bora abariki jiwe ukajengee nyumba na sio kubariki mambo yaliyo kinyume na maadili 

Askofu Kassala amesema hayo wakati akihubiri katika misa ya kitaifa ya Krisimasi iliyofanyika katika Jimbo katoliki la Geita amesema ndoa zisizo na maadili ni kwenda kinyume na maandiko ya Mungu yanayotaka wanadamu wakazaliane na kuendeleza vizazi.

Amesema binadamu anakataa uumbaji wa Mungu na kufanya mambo yaliyokatazwa huku wakitaka na kanisa liyabariki jambo ambalo amelipinga vikali.

“Binadamu amemuacha Mungu na kufanya mambo yaliyokatazwa. Binadamu amekataa uumbaji na kuendeleza uumbaji na sasa wanafanya mambo machafu yasiyompendeza Mungu, wamekuwa wakiharibu vizazi kwa kutoa mimba na sasa wanataka tubariki ndoa zisizo na maadili. Kwangu bora nibariki jiwe lakini sio uchafu huo,” amesema Askofu Kassala.

About the author

mzalendo