Featured Kitaifa

JENGA NA MIMI YATOA ZAWADI ZA KRISMASI, MWAKA MPYA 2024 KWA WATOTO YATIMA KAHAMA

Written by mzalendoeditor

Zoezi la kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment likiendelea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha  Kahama Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Manispaa ya Kahama 
Zoezi la kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 likiendelea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mvuma Simon Children Home kilichopo mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi Manispaa ya Kahama 
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Kampuni ya Uuzaji na Usambazaji wa Matofali na vifaa vya ujenzi maarufu Jenga na Mimi Investment imetoa zawadi ya mahitaji ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 pamoja na vifaa vya shule kwa watoto wanaolelewa katika Vituo vya Kulelea watoto yatima na wenye mahitaji maalum vya New Hope Orphanage Centre, Mvuma Simon Children Home na Kahama Peace Orphanage Center vilivyopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Akizungumza Desemba 23,2023 wakati wa kukabidhi mahitaji hayo (Mkono wa heri ya Krismasi), Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama, Benny Mao amesema wametoa misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa Kampuni hiyo kurudisha faida wanayopata kwa jamii.
 
Ameitaja baadhi ya misaada waliyopeleka kwenye kila kituo kuwa ni pamoja na mchele, mbuzi, Unga wa ngano, sukari,juisi, biskuti, jojo,maziwaya watoto, chumvi, Pampas, baby wipes, sabuni za unga za kufulia na mahitaji ya shule kama vile madaftari, penseli, rangi za kucholea, vichongeo, vifuto, na mikebe (Compass).

“Jenga na Mimi Investment ambayo makao yake makuu yapo mtaa wa Mwime kata ya Mwendakulima Manispaa ya Kahama ambayo inajihusisha na Uuzaji na Usambazaji wa Matofali pamoja na shughuli zote za ujenzi ipo karibu na jamii, tumekuwa tukitoa misaada katika maeneo mbalimbali tukigusa makundi mbalimbali. Tangu mwezi Januari hadi mwezi Desemba mwaka huu tumefanikiwa kutoa misaada kwa wahitaji mbalimbali na tumefunga mwaka 2023 kwa kuleta zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2024 na mahitaji ya shule kwa watoto wetu wanaolelewa kwenye vituo hivi”,amesema Mao.
 
“Ujio wetu kwenye vituo  vitatu vya kulelea watoto yatima ni sehemu ya kutimiza wajibu wetu na utamaduni wetu wa kurudisha kwa jamii kile tunachokipata. Shauku yetu ni kuona watoto hawa  170 tuliowapa mkono wa heri ya sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya wanapata furaha, wanafarijika na kusherehekea Sikukuu wakiwa na mahitaji muhimu lakini wanapofungua shule wasiwe wanyonge wawe na vifaa vya shule”,ameongeza Mao.
Wakipokea misaada hiyo na zawadi za Sikukuu, Afisa Ustawi wa Jamii wa kituo cha Mvuma Simon Children Home, Lauryne Noel, Mke wa mmiliki wa New Hope Orphanage Centre Bi. Amina Salum na Mkurugenzi wa Kahama Peace Orphanage Center bi. Halima Hamza wameishukuru Kampuni ya Jenga na Mimi Investment kwa kuwakumbuka watoto yatima na wenye mahitaji maalumu huku wakiwaomba wadau kuendelea kutembelea vituo hivyo kwani vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo chakula na mahitaji mengine.
 
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika vituo hiyo mbali na kuishukuru Kampuni ya Jenga na Mimi Investment kwa kuwapatia mahitaji hayo muhimu wameomba wadau waendelee kufika kwenye vituo hivyo ili kuwafariji watoto.
 
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwime, Stella Maige Bayungile ameipongeza Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika kata yake kwa kuwa wadau wazuri wa maendeleo kwani wamekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii hivyo kugusa makundi mbalimbali ya watu.
 
Baadhi ya Mabalozi wa Jenga na Mimi Investment akiwemo Agnes Kahabi na Joram Victor Joseph maarufu MC Ice pamoja na Meneja wa Kampuni hiyo, Sebastian Francis Mihayo wamewasihi watoto hao kusoma kwa bidii, wazingatie masomo huku wakiahidi kuwa wataendelea kutembelea vituo hivyo.
 
Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Mvuma Simon Children Home kilichopo mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi hivi sasa kina jumla ya watoto 34 na New Hope Orphanage Centre kilichopo mtaa wa Ilindi kata ya Zongomela kina jumla ya watoto 76 na Kahama Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Manispaa ya Kahama kina watoto 60.
 
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama, Benny Mao akizungumza Desemba 23,2023 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mvuma Simon Children Home kilichopo mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi Manispaa ya Kahama wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024- Picha na Kadama Malunde -Malunde 1 blog
Muonekano wa sehemu ya zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mvuma Simon Children Home kilichopo mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi Manispaa ya Kahama na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama, Benny Mao (kulia) akikabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mvuma Simon Children Home kilichopo mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi Manispaa ya Kahama 
Zoezi la kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 likiendelea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mvuma Simon Children Home kilichopo mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi Manispaa ya Kahama 
Zoezi la kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 likiendelea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mvuma Simon Children Home kilichopo mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi Manispaa ya Kahama 
Mmoja wa watoto akitoa neno la shukrani
Mmoja wa watoto akitoa neno la shukrani
Afisa Ustawi wa Jamii wa kituo cha Mvuma Simon Children Home, Lauryne Noel akizungumza wakati akipokea zawadi zilizotolewa na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment kwenye kituo hicho
Balozi wa Jenga na Mimi Investment Joram Victor Joseph maarufu MC Ice akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mvuma Simon Children Home kilichopo mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi Manispaa ya Kahama 
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwime, Stella Maige Bayungile akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mvuma Simon Children Home kilichopo mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi Manispaa ya Kahama 
Balozi wa Jenga na Mimi Investment Agnes Kahabi akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mvuma Simon Children Home kilichopo mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi Manispaa ya Kahama 
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama, Benny Mao akizungumza Desemba 23,2023 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha New Hope Orphanage Centre kilichopo mtaa wa Ilindi kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024
Muonekano wa sehemu ya zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama katika kituo cha kulelea watoto yatima cha New Hope Orphanage Centre kilichopo mtaa wa Ilindi kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama 
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama, Benny Mao (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Balozi wa Jenga na Mimi Investment Agnes Kahabi na Meneja wa Jenga na Mimi Investment, Sebastian Francis Mihayo wakikabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha cha New Hope Orphanage Centre kilichopo mtaa wa Ilindi kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama. Wa kwanza kushoto ni Mke wa mmiliki wa New Hope Orphanage Centre Bi. Amina Salum akifuatiwa na Balozi wa Jenga na Mimi Investment Joram Victor Joseph maarufu MC Ice 
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama, Benny Mao (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Balozi wa Jenga na Mimi Investment Agnes Kahabi na Meneja wa Jenga na Mimi Investment, Sebastian Francis Mihayo wakikabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha cha New Hope Orphanage Centre kilichopo mtaa wa Ilindi kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama 

Zoezi la kukabidhi zawadi likiendelea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha cha New Hope Orphanage Centre kilichopo mtaa wa Ilindi kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama
Mke wa mmiliki wa New Hope Orphanage Centre Bi. Amina Salum akizungumza wakati akipokea zawadi zilizotolewa na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment kwenye kituo hicho

Meneja wa Jenga na Mimi Investment, Sebastian Francis Mihayo akizungumza katika kituo cha kulelea watoto yatima cha New Hope Orphanage Centre

Mmoja wa watoto akitoa neno la shukrani
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama, Benny Mao akizungumza katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Kahama Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Manispaa ya Kahama wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024
Muonekano wa sehemu ya zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Kahama Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Manispaa ya Kahama na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama
Muonekano wa sehemu ya zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Kahama Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Manispaa ya Kahama na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment iliyopo katika Manispaa ya Kahama
Zoezi la kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment likiendelea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha  Kahama Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Manispaa ya Kahama 
Zoezi la kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment likiendelea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha  Kahama Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Manispaa ya Kahama 
Zoezi la kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment likiendelea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha  Kahama Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Manispaa ya Kahama 
Zoezi la kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment likiendelea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha  Kahama Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Manispaa ya Kahama 
Zoezi la kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment likiendelea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha  Kahama Peace Orphanage Center kilichopo mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Manispaa ya Kahama 
Mkurugenzi wa Kahama Peace Orphanage Center bi. Halima Hamza akizungumza wakati akipokea zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 zilizotolewa na Kampuni ya Jenga na Mimi Investment
Mkurugenzi wa Msaidizi wa Kahama Peace Orphanage Center Ustadhi Abubakar Issa akizungumza wakati Jenga na Mimi Investment ikikabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024 kwa watoto.
 
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
About the author

mzalendoeditor