Featured Kitaifa

VIONGOZI WA UMMA 2,475 KATI YA 15,762 NDIO WALIOWASILISHA TAMKO LAO LA RASILIMALI NA MADENI KWA KAMISHNA WA MAADILI NCHINI

Written by mzalendo

 

KATIBU  Ukuzaji wa Maadili Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma, Waziri Kipacha,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  kuhusu  hali ya Urejeshaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni na Mfumo wa Ujazaji Fomu za Tamko kwa njia ya Mtandao leo Desemba 21,2023 jijini Dodoma. 

KATIBU  Ukuzaji wa Maadili Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma, Waziri Kipacha,akifafanua jambo zaidi kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani)  kuhusu  hali ya Urejeshaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni na Mfumo wa Ujazaji Fomu za Tamko kwa njia ya Mtandao leo Desemba 21,2023 jijini Dodoma. 

KATIBU  Ukuzaji wa Maadili Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma, Waziri Kipacha,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani)  kuhusu  hali ya Urejeshaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni na Mfumo wa Ujazaji Fomu za Tamko kwa njia ya Mtandao leo Desemba 21,2023 jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Msaidizi Idara ya Ukuzaji Bi.Sigolwike.

Na.Alex Sonna-DODOMA

VIONGOZI wa umma 2,475  kati ya 15,762  ndio waliowasilisha tamko lao la rasilimali na madeni kwa Kamishna wa Maadili nchini ikiwa ni sawa na asilimia 16 ya viongozi wote wanaopaswa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 21,2023 jijini Dodoma Katibu ukuzaji wa maadili Ofisi ya Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, Waziri Kipacha ameelezea hali ya Urejeshaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni na Mfumo wa Ujazaji Fomu za Tamko kwa njia ya Mtandao leo Desemba 21,2023 jijini Dodoma.

Kipacha, alisema hadi kufikia juzi jumla ya viongozi 2,475 kati ya 15,762 ndio waliowasilisha matamko yao kuhusu rasilimali na madeni yao kwa Kamishna wa Maadili ya viongozi nchini.

“Hadi kufikia jana Desemba 20 mwaka huu jumla ya viongozi wa umma 2,475 kati ya viongozi 15,762 ndio waliowasilisha tamko lao la rasilimali na madeni kwa Kamishna wa Maadili hii ni sawa na asilimia 16 ya viongozi wote wanaotakiwa kuwasilisha matamko yao kwa mujibu wa sheria”amesema 

Hata hivyo amesema kuwa  zimebaki siku 10 kufika tarehe za mwisho ya viongozi hao kutakiwa kuwasilisha matamko hayo kwa Kamishna kwa mjibu wa sheria ya maadili ya  viongozi wa umma namba 13  ya mwaka 1995.

Pia amewakumbusha viongozi wote wa umma nchini kuzingatia matakwa ya katiba na sheria hiyo ya maadili kuwasilisha tamko na madeni yao kabla ya Desemba 31 mwaka huu.

Aidha amesema kuwa  kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia wameanza kupokea matamko kwa njia ya mtandao kwa kiongozi ambaye atashindwa kufika kwenye ofisi zao.

”Ujazaji wa fomu kwa njia hiyo  utawezesha viongozi kujaza fomu hizo kwa urahisi zaidi popote pale walipo iwe ndani  au nje ya nchi na unapunguza gharama.”amesema 

Hata hivyo amefafanua kuwa  kwa viongozi wapya wanapaswa kuwasilisha taarifa zao ndani ya siku 14 baada ya kuteuliwa, kupandishwa au kupandishwa cheo.

About the author

mzalendo