Featured Kitaifa

RC SHINYANGA AIPONGEZA EWURA KUANZISHA KANDA YA MAGHARIBI

Written by mzalendoeditor

Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mha. Walter Christopher (kushoto) akimkabidhi baadhi ya ripoti na machapisho ya EWURA, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Christina Mndeme (kulia), alipotembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo, kwa lengo la kuitambulisha ofisi ya Kanda na kujadili masuala mbalimbali kuhusu udhibiti wa huduma za nishati na maji.

…………..

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe.Christina Mndeme, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kuanzisha Ofisi ya Kanda ya Magharibi inayohudumia mikoa ya Tabora, Shinyanga, Katavi na Kigoma na kueleza kuwa ni njia ya kusogeza huduma karibu na wananchi na itarahisisha upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka kwa wakazi wa mkoa huo.

Mhe. Mndeme ametoa pongezi hizo kwa Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mha. Walter Christopher alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake, leo 21 Desemba 2023, kuitambulisha ofisi ya Kanda na kujadili utekelezaji wa shughuli za udhibiti wa huduma za nishati (umeme, petroli na gesi asilia) na maji na usafi wa mazingira).

“Ninawapongeza sana EWURA kwa jitihada za kusogeza ofisi karibu na wanachi, uwepo wa ofisi hii ya Kanda utaturahisishia majukumu yetu mbalimbali na huduma , ninawaahidi ushirikiano wa kutosha ili kwa pamoja tutatue changamoto zinazowakabili wananchi na kujenga nchi yetu”

Mha. Walter aliambatana na Afisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Bi. Getrude Mbiling’i na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa EWURA, Bi. Tobietha Makafu.

Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mha. Walter Christopher (kushoto) akimkabidhi baadhi ya ripoti na machapisho ya EWURA, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Christina Mndeme (kulia), alipotembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo, kwa lengo la kuitambulisha ofisi ya Kanda na kujadili masuala mbalimbali kuhusu udhibiti wa huduma za nishati na maji.

About the author

mzalendoeditor