Featured Kitaifa

EWURA, ZAMBIA ZAJADILI MASUALA YA UDHIBITI

Written by mzalendoeditor

 

Wajumbe wakiendelea na kikao kazi kilichojadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya udhibiti wa nishati kati ya Tanzania na Zambia, kilichofanyika Ofisi za EWURA, Dar es Salaam, leo 21 Desemba 2023.

……………

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo, 21 Desemba 2023, imekutana na Ujumbe wa serikali ya Zambia kwa lengo la kushauriana na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali ya kiudhibiti.

Ujumbe huo wa Zambia uliojumuisha Bodi ya Udhibiti wa Nishati (ERB), Kampuni ya Tazama Pipelines na Wizara ya Nishati, umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati nchini humo, Bw. Peter Mumba.

Ujumbe wa EWURA katika kikao hicho kilichofanyika Ofisi za EWURA jijini Dar es Salaam, umeongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Dkt. James Andilile na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile (kushoto), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Zambia, Bw. Peter Mumba, mkoba wa EWURA wenye taarifa mbali mbali za utendaji wa EWURA, baada ya kikao kifupi kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo. Bw. Mumba na ujumbe wake wameitembelea EWURA kwa lengo la kujadili masuala mbali mbali ya kiudhibiti na kubadilishana uzoefu.

Wajumbe wakiendelea na kikao kazi kilichojadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya udhibiti wa nishati kati ya Tanzania na Zambia, kilichofanyika Ofisi za EWURA, Dar es Salaam, leo 21 Desemba 2023.

About the author

mzalendoeditor