Featured Michezo

SIMBA SC YAICHAPA KAGERA SUGAR LIGI KUU

Written by mzalendoeditor

SIMBA SC ikiwa na  Kocha  Abdelhak Benchikha imepata  ushindi wa kwanza baada ya kuichapa mabao 3_0 Kagera Sugar uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kipindi Cha kwanza Simba ilienda mapumziko ikiwa na bao moja lililofungwa na  Saido Ntibazonkiza kwa penalti dakika ya 45.

Kipindi Cha pili Simba walipata mabao mawili kupitia kwa ( Sadio Kanoute  dakika ya 75 na John Bocco dakika ya  90.

Kwa ushindu huo Simba imefikisha pointi 22 baada ya mechi tisa na kupanda hadi nafasi ya tatu ambapo imetanguliwa na kinara Azam na Yanga ya pili katika msimamo.

About the author

mzalendoeditor