Featured Kitaifa

NELSON MANDELA NI KITOVU CHA UBUNIFU NA TEKNOLOJIA 

Written by mzalendo

 

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo (wa kwanza kulia) akipata maelezo kuhusu utafiti wa funza lishe kutoka kwa Mtafiti Bi. A kompyuta yenye uwezo mkubwa wa kuchakata data kwa kasi kubwa (Param Kilimanjaro Super Computer) ziza Konyo (Kushoto) alipotembelea Kituo cha Atamizi (Incubation Centre) wakati wa ziara ya kikazi Disemba 14,2023.

………………

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu wa Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya maendeleo ya nchi hivyo imewekeza miundombinu wezeshi katika Taasisi za kielimu zilizojikita katika nyanja hizo ikiwemo Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo Desemba 14, 2023 Jijini Arusha wakati wa ziara ya kikazi katika taasisi hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofanywa na taasisi hiyo.

 

Profesa Carolyne aliongeza kuwa, Serikali inawekeza zaidi katika eneo la kibiashara kuhakikisha kwamba Teknolojia zote zilizozalishwa na watafiti zinaingia sokoni kwa kuangalia mazingira ya biashara kupitia kampuni tanzu au kushirikisha na wadau wengine.

 

“Kupitia costech serikali huwa inatenga fedha kila mwaka kusaidia kuboresha Teknolojia mbalimbali ambazo zimezalishwa na watafiti wetu na wabunifu mbalimbali ili kuzifikia katika hali ambayo inaridhisha kuingia sokoni kwa ajili ya kutatua changamoto za kijamii”

 

Aidha, Professa Carolyne aliongeza kuwa katika sekta ya elimu ina ajenda ya kufanya utalii wa elimu kwa kuwavutia watu mbalimbali kuweza kutembelea Taasisi za elimu ili kujifunza masuala ya bunifu na Teknolojia mbalimbali zilizopo katika sekta mbalimbali.

“Wengi wetu wakienda nje ya nchi wanapenda kufanya utalii kwenye vyuo vya elimu au Taasisi za utafiti tunataka na sisi Tanzania tuwezeshe utalii wa kielimu na hivyo kuongeza idadi ya watalii watakotembelea nchi yetu” alisema Professa. Carolyne Nombo

 Naye Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, lengo la ziara ya Katibu Mkuu Professa Carolyne ni kujionea utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazotokelezwa na Taasisi hiyo kwa kutembelea Maabara za kufundishia na Utafiti pamoja na Kituo cha Atamizi kuona bunifu mbalimbali zinazozalishwa.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo (kulia) akiongea na Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (hawapo katika picha), wakati wa ziara ya kikazi katika Taasisi hiyo Disemba 14,2023 jijini Arusha, Kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo(kulia) akiongea na Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, katika ziara ya kikazi katika Taasisi hiyo Disemba 14, 2023 jijini Arusha.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa Mimea Tiba (kulia) alipotembelea Maabara ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, wakati wa ziara ya kikazi  Disemba 14,2023 jijini Arusha.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo (wa kwanza kulia) akipata maelezo kuhusu utafiti wa funza lishe kutoka kwa Mtafiti Bi. A kompyuta yenye uwezo mkubwa wa kuchakata data kwa kasi kubwa (Param Kilimanjaro Super Computer) ziza Konyo (Kushoto) alipotembelea Kituo cha Atamizi (Incubation Centre) wakati wa ziara ya kikazi Disemba 14,2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo(katikati) akipata maelezo kuhusu kompyuta yenye uwezo mkubwa wa kuchakata data kwa kasi kubwa (Param Kilimanjaro Super Computer) kutoka kwa Afisa Tehama Bw. Mdoe Mwamunyange (Kulia), wakati wa ziara ya kikazi katika Taasisi hiyo Disemba 14,2023 jijini Arusha, Kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela , wakati wa ziara ya kikazi katika Taasisi hiyo Disemba 14,2023 jijini Arusha.

About the author

mzalendo