Featured Michezo

SIMBA SC YACHAPWA NA KUSHIKA MKIA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Simba SC imeshushwa hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa kundi B baada ya kufungwa bao 1-0 na Wydad Casablanca katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika  uliochezwa Uwanja wa Stade Mohamed V nchini Morocco

Wenyeji walipata bao dakika za jioni 90+3 ambalo limewapa Matumaini na kufikisha pointi tatu huku Simba akishika nafasi ya nne na pointi zake mbili baada ya michezo mitatu.

ASEC Mimosas anaongoza Kundi B akiwa na pointi saba baada ya kuifunga Jwaneng Galaxy   huku Jwaneng akishika nafasi ya pili na pointi nne.

Timu hizo zinatarajia kucheza mechi ya marudio Desemba 19, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

About the author

mzalendoeditor