Featured Kimataifa

DKT. JINGU ASHIRIKI UZINDUZI WA MKUTANO WA SADC WA MAWAZIRI WA AFYA AKIMUWAKILISHA WAZIRI UMMY

Written by mzalendoeditor

Na WAF – Luanda, Angola.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu amemuwakilisha Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu katika mkutano wa Jumuiya ya SADC wa Mawaziri wa Afya na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya UKIMWI unaoendelea Luanda Nchini Angola kuanzia Novemba 25 – 29,2023.
Awali Dkt. Jingu ameshiriki Uzinduzi wa Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya matembezi na maandamano kwa washiriki kubeba mabango yenye jumbe mbalimbali zenye Kaulimbiu isemayo “Community led” uzinduzi ambao ni sehemu ya nchi za Jumuiya ya SADC kushirikiana na nchi mwenyeji kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI miongoni mwa nchi wanachama.

Katika Mkutano huo, Mawaziri na wawakilishi wao wanatarajiwa kujadili masuala ya afya yenye lengo la kuchangia katika kufanikisha uboreshaji wa hali ya maisha ya wananchi katika nchi wanachama, kuchunguza hali ya utekelezaji wa maamuzi ya vikao vyao vya pamoja vya awali na kupitia hali ya afya katika ukanda wa SADC.

Mawaziri wa afya pia watahudhuria maadhimisho ya Siku ya Malaria ya SADC Luanda – Angola tarehe 29 Novemba 2023.

About the author

mzalendoeditor