Wanawake waliohudhuria kampeni ya kutokomeza Malaria ya Barrick Bulyanhulu katika kijiji cha Lwakabanga,wakifurahia baada ya kukabidhiwa vyandarua vyenye dawa vya kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria. kampeni hiyo inaendelea kwa kipindi cha wiki moja wilayani Msalala mkoani Shinyanga.
Wanafunzi waliohudhuria kampeni ya kutokomeza Malaria ya Barrick Bulyanhulu katika kijiji cha Lwakabanga, wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa kampuni hiyo baada ya kukabidhiwa vyandarua vyenye dawa vya kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria.kampeni hiyo inaendelea kwa kipindi cha wiki moja wilayani Msalala mkoani Shinyanga.
Baadhi ya wazee wa kijiji cha Busulwangiri wakifurahia vyandaruabwalivyozawadiwa katika kampeni hiyo.
Wawakilishi wa Barrick Bulyanhulu wakiwa na mabango wakiendela na kampeni ya kutokomeza Malaria inayoendelea.
Watoto wakisikiliza kampeni dhidi ya Malaria kabla ya kukabidhiwa vyandarua.
Wawakilishi wa Barrick Bulyanhulu wakigawa vyandarua kwa wananchi.
Mmoja wa wakazi wa Lwakabanga akifurahia chandarua
Wawakilishi wa Barrick Bulyanhulu wakigawa vyandarua kwa wananchi.
Mwakilishi wa Barrick Bulyanhulu akifanya uhamasishaji katika kampeni hiyo.
Wanafunzi nao hawabaki nyuma kushiriki kampeni hii muhimu ya afya.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Busulwangiri wakifuatilia kampeni hiyo.
#Wanawake,wazee na vijana wanufaika na elimu ya tokomeza Malaria
***
Kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria inayoendelea, iliyozinduliwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, karibuni yenye kauli mbiu ya ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI ,WEWE NA SISI SOTE inazidi kuwafikia wananchi wengi wilayani Msalala ambapo wengi wanajitokeza kupata elimu dhidi ya Malaria katika mikutano ya hadhara na kugawiwa vyandarua kwa kila kaya.
Baada ya kukamilika zoezi la kugawa vyandarua na kutoa elimu litaanza zoezi la kunyunyizia dawa kwenye mazalia ya mbu kwenye makazi ya watu sambamba na kwenye madimbwi zaidi ya 80 kwenye vijiji 8 vya kata za Bugarama na Bulyanhulu.
Akitoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa Malaria, kwa wananchi wa vijiji vya Busulwangiri na Lwabakanga, viliyopo kata ya Bulyanhulu, Halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama, Kaimu Mganga Mkuu na Mratibu wa Malaria Dk. Martine Mazigwa, amesema kulingana na tafiti zilizofanywa na kugundulika kuwa madimbwi hayo kuwa na Mbu wengi hivyo ni Muhimu kunyunyuzia dawa ili kuiweka jamii katika mazingira salama ya kujingika na Maambukizi ya Ugonjwa huo hatari.
“Tumefanya utafiti katika madimbwi yetu haya na kugundua Mbu wengi sana wanapatikana hivyo tukaona ni busara kunyunyuzia dawa ila niwatoe wasiwasi dawa hii haitakuwa na Madhara yoyote kwa binadamu wala mifugo yetu hivyo tunaomba ushirikiano wenu tukifika katika Maeneo yenu”, amesema Dkt. Mazigwa.
Akiongea kwa niaba ya wananchi, Katarina Ernest, mkazi wa kijiji cha Busulwangiri amesema kampeni hii inayoendelea imeleta mabadiliko kwenye jamii kwani sasa wanaelewa njia sahihi za kujikinga pamoja na kujua dalili za ugonjwa wa Malaria.
Naye Mbogo Wilson Mbogo, mkazi wa kijiji cha Lwakabanga amesema kuwa kampeni hii ni muhimu kwa kuwa itasaidia kutokomeza vifo vitokanavyo na Malaria hususani kwa akina mama na watoto na aliishukuru Barrick kwa kuleta elimu ya kupambana na Malaria kwa vitendo kwenye jamii.
“Tunaishukuru serikali ya Halmashauri yetu pamoja na hawa ndugu zetu wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kutukumbuka sisi wananchi ambao tupo kwenye hatari kubwa ya kupatwa na ugonjwa huu wa malaria ,leo tumepata elimu ya kutosha lakini tumepata na hivi vyandarua sasa tuna imani familia zetu zitakuwa salama”. Wananchi hao”, wamesema
Mwakilishi wa Mgodi wa Barick Bulyanhulu katika kampeni hiyo Stella Kuyonga, ametoa rai kwa wananchi kutumia vyandarua wanavyoendelea kupewa kujikinga na mbu na siyo kuvitumia katika matumizi yasiyofaa kama kufungia kuku.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo karibuni, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare, amesema kuwa Barrick itaendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali za kuleta maendeleo kwa wananchi sambamba na kuhakikisha wanakuwa na afya bora.
Sangare amesema kupitia kampeni hii Barrick Bulyanhulu itawezesha kaya zipatazo 17,500 kufikiwa kwa makazi yao kunyunyiziwa dawa za kuua mazalio ya mbu sambamba kugawiwa vyandarua.