Featured Kitaifa

SUA CEO WAKUTANA KUJADILI MWENENDO WA CHUO

Written by mzalendo
Na Farida Mangube  Morogoro 
Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa mara ya kwanza katika wiki ya Majalisi imekutana na wakurugenzi watendaji wa wataasisi na Kampuni mbalimbali za umma na Binafsi ambao wamewahi kusoma SUA katika vipindi tofauti toka kuanzishwa kwake mwaka 1984 kwa lengo la kuimarisha mashirikiano.
Akizungumza katika kikao hicho Kilichofanyika Kampasi Mkuu ya Edward Moringe mkoani Morogoro Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amesema lengo la Chuo ni kufanya utambuzi wa wahitimu wake wapo wapi, wanafanya nini na wanawezaje kukisaidia Chuo katika kuboresha mambo mabalimbali.
Amesema kuna wahitimu zaidi ya elfu tano waliosoma SUA lakini Chuo kimeona kianza na wachache ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye nchini hivyo kupitia wao watakisaidia Chuo kuweza kuongeza ubunifu katika ufundishaji na kuwaanda wahitimu wa sasa kuendana na soko la ajira na kuweza kujiajili.
Kwa upande wake Naibu Makamu wa Chuo Taaluma,Utafiti, na Ushauri wa Kitaaluma Chuo Kikuu cha Sokeine cha Kilimo SUA Prof. Maulid Mwatawala amesema kwa sasa SUA mambo yameadilika tofauti na hapo awali, kuanzia kwenye udahili ambapo umeongeza kutoka anafunzi 300 hadi Elfu kumi na sita, ongezeko la Ndaki  kutoka 3 hadi 7 na kufanya kuendelea kukua,
Aidha amesema katika kipindi ambacho Chuo kinapitia mitaala yake kuna  umuhimu ukubwa sana wa kushirikisha Alumin wake ambao wanakijua vizuri chuo hivyo watakuwa na mchango mkubwa utakaosaidia maboresho/mabadiriko ya mitaala.
Nae Naibu Kataibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Daniel Mushi ambaye pia ni Alumin wa Chuo Kikuu SUA ameipongeza menejimenti ya Chuo kwa kuendelea kuwa katika nafasi zuri ya kukuza ujuzi kwa wahitimu ambao wamekuwa na uwezo wa kujiajiri.
Nae Rais wa Majalisi Dkt. Reymond J Salanga amemuhakikishia Makamu Mkuu wa Chuo na Menenejimenti nzima kwamba Alumin wapo tayari kushirikiana na Chuo katika kuboresha mambo mbalimbali kwa kutoa michango muda wote watakapohitajika.
Aidha amesema kunapotokea changamoto yeyote ambazo zinahitaji ushauri Alumin wanatakiwa kuwa chachu ya kutatua changamoto hiyo, kuja na ushauri hasa kwenye maboresho/mabadiriko ya mitaala
Katika kikao hicho cha siku moja kati ya Menejimenti ya Chuo Kikuu SUA na wakurugenzi wa Taasisi na kamapuni ambao wamesoma SUA kimetoka  na maadhimio ya kujengwa kwa Ofisi ya Majalisi (Convection) ambayo itaghalimu zaidi ya Bil. 1, atayari zaidi ya milioni 15 zimepatikana katika kikao hicho huku Chuo kikichangia milioni 500.

About the author

mzalendo