Featured Kitaifa

BARRICK BULYANHULU YAZINDUA KAMPENI YA ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI ,WEWE NA SISI SOTE

Written by mzalendo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Khamis Katimba, na Meneja Mkuu wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza Malaria ya Barrick inayojulikana kama ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI ,WEWE NA SISI SOTE
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Khamis Katimba, (wa nne kutoka kulia) akiwa na Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakionyesha vipeperushi vyenye ujumbe wa kutokomeza Malaria wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza Malaria inayojulikana kama ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI ,WEWE NA SISI SOTE uliofanyika eneo la Bugarama wilayani Msalala Mkoanin Shinyanga mwishoni mwa wiki.Wa tano kulia ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Cheick Sangare.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala, Khamis Katimba,akiongea katika hafla hiyo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Cheick Sangare akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Baadhi ya wageni wakiwa meza kuu wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
Baadhi ya Waendesha pikipiki wa kitongoji cha Bugarama wakionyesha vipeperushi vyenye ujumbe wa kutokomeza Malaria wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza Malaria ya Barrick Bulyanhulu inayojulikana kama ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI ,WEWE NA SISI SOTE
Afisa Mawasiliano na mahusiano ya jamii wa Barrick Bulyanhulu,Zuwena Senkondo akigawa vyandarua kwa wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Mmoja wa wakazi wa Bugarama aliyehudhuria uzinduzi huo akifurahia zawadi ya chandarua aliyopatiwa kutoka Barrick Bulyanhulu.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzunduzi huo wakifuatilia matukio.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzunduzi huo wakifuatilia matukio.
 
****
 
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo wilayani Msalala mkoani Shinyanga umezindua kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria ijulikanayo kama ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI ,WEWE NA SISI SOTE.
 
Uzinduzi huo uliofanyika katika kata ya Bugarama umehudhuriwa na wananchi kutoka vitongoji mbalimbali kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi huo,wafanyakazi wa Barrick na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Msalal, Khamis Katimba ambaye alikuwa ni Mgeni Rasmi.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Cheick Sangare, amesema kuwa Barrick itaendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali za kuleta maendeleo kwa wananchi sambamba na kuhakikisha wanakuwa na afya bora.
 
“Afya ni suala la muhimu katika jamii yoyote ile ndio maana Barrick tumekuja na kampeni ya kutokomeza ugonjwa hatari wa Malaria ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambao wamekuwa wahanga wakubwa wa ugonjwa huu na nina imani sote tukuingana pamoja tutafanikiwa kutokomeza ugonjwa huu” , amesema Sangare.
 
Sangare, alisema kupitia kampeni hii Barrick Bulyanhulu, itawezesha kaya zipatazo 17,500 kufikiwa katika makazi yao kwa kunyunyiziwa dawa za kuua mazalio ya mbu sambamba kugawiwa vyandarua .
 
Akitoa salamu kwa niaba ya Serikali katika hafla hiyo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Msalala Khamis Katimba, ametoa rai kwa wananchi wataofikiwa na kampeni hiyo kutoa ushirikiano kwa watoa huduma watakaofika katika kaya zao pia ameupongeza mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuzindua kampeni hiyo ambayo inaenda sambamba na jitihada za Serikali za kuboresha sekta ya afya na kutokomeza magonjwa mbalimbali kwenye jamii.
 
Akitoa tathimini ya maambukizi ya ugonjwa huo katika kata mbili ya Bugarama na Bulyanhulu, Dkt. Martin Mazigwa, ambaye ni Mratibu wa Malaria katika eneo hilo amesema kiwango cha maambukizi kimepungua kati ya mwaka 2020-2023 kutoka asilimia 29.4 hadi Asilimia 18.9 katika kata hizo mbili.
 

About the author

mzalendo