Featured Kitaifa

BALOZI NJALIKAI  ATETA  NA RAIS WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA WATU NA BINADAMU

Written by mzalendo

Leo tarehe 19 Novemba 2023, nimempokea na kufanya naye mazungumzo Mhe. Jaji Iman Aboud, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Watu na Binadamu katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Algiers.

Mhe. Jaji Aboud anaongoza Mkutano wa 71 wa Mahakama hiyo unaofanyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria kuanzia tarehe 06 Novemba 2023 na unatarajiwa kukamilika tarehe 04 Desemba 2023.

Mkutano huo, utakapokamilika unatarajiwa kutoa hukumu ya mashauri takriban 9 ya kimahakama.

About the author

mzalendo