Featured Kimataifa

RAIS WA ROMANIA AWASILI ZANZIBAR

Written by mzalendo

Rais wa Romania, Mhe. Klaus Iohannis amewasili Zanzibar kwa Boti ya AZAM na kupokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi- Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali. 

Akiwa Zanzibar, Rais Iohannis atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na baadaye kutembelea Mji Mkongwe ambao ni moja kati ya vivutio vikubwa vya utalii duniani. Rais Iohannis ambaye yupo nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku nne ataondoka nchini tarehe 19 Novemba 2023.

About the author

mzalendo