Featured Kitaifa

DKT.BITEKO AWASILI TABORA KUSHIRIKI SHEREHE ZA KUMPONGEZA ASKOFU MKUU MSTAAFU PAUL RUZOKA 

Written by mzalendo

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili mkoani Tabora ambapo kesho atashiriki katika Sherehe za kumpongeza Mhasham Askofu Mkuu Mstaafu Paul  R. Ruzoka na kumtakia Matashi mema Askofu Mkuu Mpya wa Tabora,  Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa. Sherehe zitafanyika katika Jimbo Kuu  Kanisa Katoliki Tabora.

Mara baada ya kuwasili mkoani Tabora, Dkt. Biteko alipokelewa na Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Batilda Burian.

About the author

mzalendo