Featured Kitaifa

ZAIDI YA BILIONI TISA ZATENGWA KUWEZESHA BUNIFU NA TEKNOLOJIA

Written by mzalendo

 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga  akihutubia  wageni wakati wa ufunguzi wa Hafla wa kuadhimisha miaka sita ya kituo cha Umahiri cha Tehama cha Afrika Mashariki (CENIT@EA) kilichopo katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Novemba 17,2023 jijini Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula  akitoa neno la ukaribisho wakati wa ufunguzi wa Hafla wa kuadhimisha miaka sita ya kituo cha Umahiri cha Tehama cha Afrika Mashariki (CENIT@EA) kilichopo katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Novemba 17,2023 jijini Arusha.

Katibu Mtendaji wa Umoja wa Vyuo Vikuu Afrika Mashariki (IUCEA) Prof. Gaspard Banyakimbona  akiongea wakati  wa  Halfa ya kusherekea miaka sita ya Kituo cha Umahiri cha Tehama cha Afrika Mashariki (CENIT@EA) kilichopo katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Novemba 17,2023 jijini Arusha.

Wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa halfa ya kusherekea miaka sita ya Kituo cha Umahiri cha Tehama cha Africa Mashariki  (CENIT@EA) kilichopo katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia Ya Nelson Mandela yaliyofanyika Novemba 17,2023 jijini Arusha.

Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka sita ya Kituo cha Umahiri cha Tehama cha Afrika Mashariki (CENIT@EA)  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga  (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wahadhili kutoka  Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Novemba 17, 2023 Jijini Arusha.

 Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka sita ya Kituo cha Umahiri cha Tehama cha Afrika Mashariki  (CENIT@EA) Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga  (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi waliopata fursa ya kufadhiliwa katika kituo hicho kilichopo katika  Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Novemba 17, 2023 Jijini Arusha.

………………..

Serikali imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 9 kwa Mwaka wa fedha 23/24 ili kuwezesha bunifu na teknolojia mbalimbali zilizoibuliwa ili kuziweze kuwa bidhaa na kuingia sokoni kwa ajili ya kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga Novemba 17,2023 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kuadhimisha miaka sita ya kituo cha Umahiri cha Tehama cha Afrika Mashariki kilichopo katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.

 

 Mhe. Kipanga ameeleza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa kwenye ujenzi wa miundombinu,  na kusomesha  wataalam wengi katika nyanja mbalimbali 

“Sisi kama Serikali  wajibu  wetu ni kuhakikisha tunatengeneza mazingira wezeshi kwa kuweka miundombinu sawa,  pamoja na kutengeneza sera zitakazosimamia  progamu hizi ili kuendelea kuzalisha   wataalam wengi zaidi wa TEHAMA kwa ukanda wa Afrika Mashariki” Naibu Waziri Mhe. Omary Kipanga

Naye Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza  kuwa,  kituo hicho cha Umahiri katika Tehama  kwa upande wa Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka sita kimefanikiwa kutoa wahitimu 136 kutoka katika nchi za wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

“jambo zuri ni kuwa wahitumu hawa ,  mbali na kuhitimu masomo yao wameweza kuibua bunifu mbalimbali ambazo kwa kiasi kikubwa zimechangia katika kutatua changamoto za jamii” Anasema Prof. Kipanyula 

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Umoja wa Vyuo Vikuu Afrika Mashariki (IUCEA) Prof. Gaspard Banyakimbona  amesema kuwa, kama umoja wa vyuo vikuu ni utahakikisha unandeleza ushirikiano katika kutoa elimu katika eneo la kidigitali katika kuendana na kasi ya mapinduzi ya viwanda ya nne na ya tano  kwa upande wa teknolojia.

Halfa hiyo ya kuadhimisha miaka sita ya Kituo hicho  kinachofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani  kupitia kampuni ya Gesellschaft fur Internationale Zusammenarbeit (GIZ) chini ya uratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki imeshirikisha wadau kutoka nchi mbalimbali.

About the author

mzalendo