Featured Kitaifa

WANANCHI WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI SIMIYU, MABILIONI YA FEDHA YATOLEWA NA RAIS SAMIA

Written by mzalendo

Wananchi wa Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Busega wameoneshwa kuridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayotekelezw na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassabln ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Hayo yamejidhiirisha wakati ambapo Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Cde. Paul Makonda aliposimama kuzungumza na Wananchi hao Wilayani Busega ambapo waliwakilishwa na Mbunge wao wa Busega Mhe. Saimon Songe aliyeeleza namna fedha nyingi zimeletwa na Serikali ya Mama Samia kama ifuatavyo;

> Tsh Bilioni 400 kwa Ujenzi wa Chuo cha Veta.
> Tsh Bilioni 2.287 kwa miradi ya barabara kila kata.
> Serikali imejenga Vituo vya Afya 4 kwa wakati mmoja vyenye jumla ya Tsh Bilioni 2.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt. Yahya Nawanda, ameainisha fedha mbalimbali kiujumla wake katika miradi mbalimbali kama ifuatavyo;

> Zaidi ya Tsh Bilioni 444 kwa Mradi wa Maji Busega – Bariadi – Maswa hadi Meatu.
> Zaidi ya Tsh Bilioni 60 kwa ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme kujengwa Bariadi katika njia kuu ya kuunganisha na Shinyanga.

Vilevile RC Mhe. Dkt. Nawanda amebainisha kuwa tayari wameshaandika barua kuomba fedha Tsh Bilioni 6 kwaajili ya Ujenzi wa Soko (Tsh B 3.4) na Stendi Busega (Tsh B 2.6) na kumuomba Mwenezi Makonda kusaidia kusukuma jambo hilo.

Akizungumza na Wananchi hao, Mwenezi Makonda amesema Rais Samia kwa kazi hii kubwa anayoendelea kuifanya maana yake ameweka deni kanda ya ziwa kwani ridhaa ya kuongoza 2020/25 matokeo yake chanya yanaonekana sasa ni kumuombea kwa Mungu ilikusudi 2025 katika uchaguzi Mkuu nasi wana Kanda ya ziwa tulipe deni.

Aidha, amemwakikishia Mkuu wa Mkoa Simiyu kwamba Chama kitaweka msukumo mkubwa katika kuhakikisha fedha walizoomba zinapatikana kwa haraka.

About the author

mzalendo