Featured Kitaifa

NHIF YAPEWA MIEZI 3 KUBORESHA MIFUMO YA TEHAMA

Written by mzalendo

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel,akijibu  swali Namba 149 kwa Niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, kutoka kwa Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine John Kanyasu aliyeuliza kwa nini NHIF inazuia matibabu ya baadhi ya wagonjwa wenye Bima za Afya wakiwa Hospitali leo Novemba 10,2023 bungeni jijini Dodoma.

Na. WAF, Dodoma

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameitaka Menejimenti ya Mfuko wa Bima ya Afya katika kipindi cha miezi mitatu ihakikishe inaboresha mifumo ya Tehama itakayoweza kuondoa usumbufu na pia kudhibiti udanganyifu pasipo kuwa kero kwa wanufaika wa Mfuko.

Dkt. Mollel ametoa agizo hilo leo wakati akijibu swali Namba 149 kwa Niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, kutoka kwa Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine John Kanyasu aliyeuliza kwa nini NHIF inazuia matibabu ya baadhi ya wagonjwa wenye Bima za Afya wakiwa Hospitali.

“Ni kweli kulikuwa na zoezi la uhakiki wa uhalali wa wanufaika wa mfuko wa bima ya Afya, zoezi hilo lilileta usumbufu ambao ungeweza kuzuilika kama wahakiki hao wangetumika wataalamu wenye miiko ya taaluma ya tiba”, ameeleza Dkt. Mollel

Dkt. Mollel amesema Serikali ilipopata malalamiko hayo ilifuatilia mara moja na kufanya maboresho ambayo yaliyoondoa usumbufu kwa wateja na wateja kuendelea kupata Huduma kwa ufasaha.

Kwa upande wake Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine John Kanyasu, amempongeza na kufurahishwa Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel kwa kujibu maswali kwa ukweli

About the author

mzalendo