Featured Kitaifa

MWONGOZO WA KITAIFA WA KILIMO IKOLOJIA HAI WAZINDULIWA DODOMA

Written by mzalendo

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde,akizindua Mwongozo wa Kitaifa wa Kilimo Ikolojia Hai  leo Novemba 8,2023  wakati wa   Mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo Ikolojia Hai unaofanyika  kwa siku mbili jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde,akizungumza leo Novemba 8,2023  wakati   akifungua Mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo Ikolojia Hai unaofanyika  kwa siku mbili jijini Dodoma.

 Mwenyekiti Kamati ya wataalamu NEOAS (Mkakati wa taifa wa kilimo ikolojia hai) Bw.Revelian S. Ngaiza,akizungumza  wakati  wa  Mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo Ikolojia Hai unaofanyika  kwa siku mbili jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde,akikagua mabanda mbalimbali  leo Novemba 8,2023  wakati   wa Mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo Ikolojia Hai unaofanyika  kwa siku mbili jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde,akizindua Mwongozo wa Kitaifa wa Kilimo Ikolojia Hai  leo Novemba 8,2023  wakati wa   Mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo Ikolojia Hai unaofanyika  kwa siku mbili jijini Dodoma.

 

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  Mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo Ikolojia Hai unaofanyika  kwa siku mbili jijini Dodoma.

Na. Gideon Gregory, Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde ametoa rai kwa wadau wa kilimo nchini kuweka mipango na vipaumbele ili kuhakikisha mkakati wa kilimo Ikolojia hai unatekelezwa kwa ufanisi na kuleta tija katika jamii.

Mhe. Silinde ametoa rai hiyo leo Novemba 8,2023 Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo Ikolojia Hai ambao unatarajia kufanyika kwa siku mbili huku wadau mbalimbali wa kilimo wakishiriki katika mkuatano huo.

Amesema pamoja na kujadili malengo mbalimbali mkutano huo utashuhudia uzinduzi wa mkakati wa kilimo Ikolojia Hai kupitia wadau wote ndani na nje ya Tanzania waliochangia rasilimali mbalimbali zilizopelekea ukamilishaji wa zoezi la uandaaji wa mikakati wa huo.

“Mkutano huu ukiwa umehudhuriwa na wadau wengi taasisi za serikali, taasisi zisizo za kiserekali, wabia wa maendeleo wa ndani na nje ya Tanzania, sekta binafsi na wawakilishi wa bara unaenda kutafakari kwa kina ili kutekeleza kwa vitendo jitihada za kuendeleza kilimo Ikolojia hai katika taifa letu”amesema Silinde..

Kwa upande wa kiongozi wa mradi kitovu cha Agroecology nchini Prof. Dismas Mwaseba amesema kilimo cha kisasa hakijafanikiwa kwani bado kuna tatizo la njaa nchini kutokana na mfumo wa kilimo hivyo kilimo Ikolojia kina fursa kubwa kwasababu ya faida inayotokana na kilimo chenyewe ambacho kinazingatia maswala ya kijamii, kiuchumi na mazingira pia.

“Kuna umuhimu wa kuendeleza majidiliano na serikali ili kuwa na sera rafiki ambazo zitasaidia muendelezo wa kilimo Ikolojia nchini Tanzania kwa maana kwamba ili uweze kueneza kilimo hiki kuna jambo kubwa linahitajika, tunahitaji msukumo wa kitaasisi ninaposema msukumo wa kitaasisi hapa nina maana maswala yote yanayohusiana na sera, mipango, sheria mbalimbali zinahitajika ili tuweze kufanikiwa katika swala hili,”amesema Prof. Mwaseba.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Biovision African Trust Dkt. David Amudavi amesema kilimo hai Ikolojia ni maisha pia ni chakula na wanahitaji kuona Afrika ikiwa mahali salama na watu wanaishi maisha na mazingira ya afya nzuri kupitia kilimo cha Ikolojia.

“Kilimo hai kimewekwa nguli na viongozi wetu wa nchi zote za Afrika. Mwaka wa 2010 mawaziri wote wa kilimo walithibitisha sheria ya kusema kwamba kilimo hai kipatiwe nafasi katika nchi zetu zote za Afrika na mwezi January 2030 viongozi wataweka sahihi,” amesema Dkt. Anudavi.

About the author

mzalendo