Featured Kitaifa

SERIKALI INAANGALIA UWEZEKANO WA KUFANYA VIKAO VYA SMT NA SMZ KUWA VYA KISHERIA

Written by mzalendo

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mwera Mhe. Zahor Mohammed Haji kuhusu utaratibu wa vikao hivi umetumika kwa mafanikio makubwa na kuhakikisha changamoto nyingi zinatatuliwa, bungeni jijini Dodoma leo Novemba 3, 2023.

……………….

Serikali imesema inaangalia uwezekano wa kufanya vikao vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuwa vya kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Novemba 3, 2023.

Amesema kuwa changamoto zote za Muungano zimekuwa zikitatuliwa na kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya majadiliano na maridhiano, utaratibu ambaoi umekuwa wa mafanikio makubwa.

Mhe. Khamis amesema kuwa katika utatuzi wa changamoto hizo umeandaliwa utaratibu wa vikao vya Kamati ya Pamoja ya SJMT na SMZ wa kushughulikia masuala ya Muungano wa Aprili 2019.

Akiendelea kujibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mwera Mhe. Zahor Mohammed Haji, Naibu Waziri Khamis amesema kuwa utaratibu wa vikao hivi umetumika kwa mafanikio makubwa na kuhakikisha changamoto nyingi zinatatuliwa.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo Novemba 3, 2023.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mwera Mhe. Zahor Mohammed Haji kuhusu utaratibu wa vikao hivi umetumika kwa mafanikio makubwa na kuhakikisha changamoto nyingi zinatatuliwa, bungeni jijini Dodoma leo Novemba 3, 2023.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Naibu Waziri wake Mhe. Khamis Hamza Khamis wakifuatilia kipindi maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo Novemba 3, 2023.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi wa Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kipindi maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo Novemba 3, 2023.

About the author

mzalendo