Featured Kitaifa

KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LIMITED YASHIRIKI MAONESHO YA SIDO NJOMBE

Written by mzalendo

 

Ferdinand Shayo ,Njombe.
 
Kampuni ya Mati Super Brands Limited imeshiriki maonesho ya nne ya Sido kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Saba saba Mkoani Njombe ambapo mamia ya Wakazi wa mkoa huo wametembelea banda la kampuni hiyo na kujionea bidhaa mbali mbali zinazozalishwa na kampuni hiyo ya kutengeneza vinywaji vikali vyenye ubora ikiwemo Strong Dry Gin,Tanzanite Primeum Vodka,Sed Pineapple na Tai Origional potable spirit.
 
Meneja Chapa wa Kampuni hiyo Izack Piganio amesema kuwa maonesho hayo yamewakutanisha na wateja wa bidhaa zao moja kwa moja Pamoja na wateja wapya waliofika na kuona bidhaa zao na kuvutiwa nazo .
 
Piganio amesema kuwa maonesho hayo ni fursa ya kibiashara kwa kampuni hiyo na wajasiriamali wengine katika kutangaza bidhaa zao zenye ubora wa kitaifa na kimataifa.

 

 

“Tunapenda kuwapongeza waandaaji wa maonesho haya kwa kuwakutanisha wajasiriamali kutoka kila pembe ya Tanzania kuja kujifunza teknolojia mbali mbali lakini pia kutafuta fursa za masoko ya bidhaa wanazozizalisha” Anaeleza Piganio
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SIDO Musa Nyansigwa amesema wataendelea kuandaa maonesho mbali mbali ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa viwanda vikubwa na vidogo kuhakikisha wanaonyesha bidhaa zao na kupata masoko.
 
“Tunaipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa viwanda pamoja na kuijengea uwezo SIDO ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuendeleza viwanda vidogo “ Anaeleza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SIDO

About the author

mzalendo