Featured Kitaifa

WAFANYABIASHARA WA ALGERIA KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA MWAKA 2024

Written by mzalendo

Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Njalikai (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu na Afrika (Arab-African Centre for Investment and Development-CAAID), Dkt. Amine Boutalbi yaliyofanyika jijini Algiers tarehe 26 Oktoba 2023

Rais
wa Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu na Afrika (Arab-African Centre
for Investment and Development-CAAID), Dkt. Amine Boutalbi amesema kuwa CAAID
inaratibu ushiriki wa wafanyabiashara wa Algeria kwenye maonesho ya Kimataifa
ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Maonesho ya Saba Saba kwa mwaka 2024.

Amesema
hayo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman
Njalikai yaliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers
tarehe 26 Oktoba 2023.

Aidha,
Dkt. Amine Boutalbi ameahidi kuwa CAAID itashirikiana na Ubalozi wa Tanzania
nchini Algeria kutaratibu kongamano maalum la wafanyabishara wa Algeria litakalofanyika
nchini Tanzania mwaka 2024 kwa lengo la kuimarisha uwekezaji na biashara kati
ya wafanyabiashara wa nchi hizi mbili.

Kwa
upande wake, Balozi Njalikai ameahidi kuwa atashirikiana na kituo hicho ambacho
ni kiungo muhimu kati ya Ubalozi na Sekta Binafsi nchini Algeria.
 

Mhe.
Balozi amehidi pia ofisi yake itashirikiana na mamlaka za Tanzania hususan
TPSF, TIC na TANTRADE ili kufanikisha ushiriki wa wafanyabiashara wa Tanzania
kwenye makongamano ya uwekezaji na biashara yanayoandaliwa na Kituo cha CAAID
mwezi Mei 2024.

Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Njalikai akimkaribisha ofisini kwake Rais wa Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu na Afrika (Arab-African Centre for Investment and Development-CAAID), Dkt. Amine Boutalbi kwa ajili ya mazungumzo

 

Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Njalikai akiwa katika mazungumzo na Rais wa Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu na Afrika (Arab-African Centre for Investment and Development-CAAID), Dkt. Amine Boutalbi 

 

About the author

mzalendo