Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza changamoto mbalimbali zinazotolewa na wananchi wa Kipengere Wilaya ya Wang’ing’ombe mkoani Njombe wakati akiwa ziarani mkoani humo leo tarehe 27 Oktoba 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa Kipengere Wilaya ya Wang’ing’ombe mkoani Njombe wakati akiwa ziarani mkoani humo leo tarehe 27 Oktoba 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili Kijiji cha Lugenge kwaajili ya kuweka jiwe la msingi mradi wa maji kijijini hapo wakati akiwa ziarani mkoani Njombe leo tarehe 27 Oktoba 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majsafi na Usafi wa Mazingira Njombe Mhandisi John Festo kuhusu mradi wa maji wa Lugenge wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika mradi huo leo tarehe 27 Oktoba 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka jiwe la msingi mradi wa maji lugenge wakati akiwa ziarani mkoani Njombe leo tarehe 27 Oktoba 2023
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lugenge mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa maji katika Kijiji hicho akiwa ziarani mkoani Njombe leo tarehe 27 Oktoba 2023.
..………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameagiza viongozi wa Wizara ya Ardhi, Tamisemi pamoja na Mkoa wa Njombe kumaliza kwa mgogoro wa mpaka baina ya Wilaya ya Makete na Wang’ing’ombe unaosababisha changamoto kwa wananchi.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kipengere Wilayani Wang’ing’ombe akiwa ziarani mkoani Njombe leo tarehe 27 Oktoba 2023. Amesema ili kulinda na kudumisha amani kwa wananchi ni muhimu kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo hizo za mipaka.
Aidha Makamu wa Rais ameigiza Wizara ya Viwanda na Biashara kushughulikia changamoto ya vipimo visivyo sahihi katika mazao ya kilimo (lumbesa) kuanzia katika masoko muhimu makubwa ya mazao hayo. Amesema changamoto hiyo imekuwa ikiathiri wakulima na kuitaka Wizara kuweka mpango kazi unaotekelezeka katika kuondoa adha hiyo.
Akiwa katika Wilaya ya Wang’ing’ombe Makamu wa Rais amewaasa wananchi wa wilaya hiyo kuzingatia lishe ili kuwa na kizazi kitakachokuwa na afya njema ya mwili na akili. Pia amewasihi kujiepusha na magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ukimwi, kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya, kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kukomesha mauaji na ubakaji pamoja na kutumia vema vyombo vya moto ili kuepusha ajali zinazogharimu Maisha ya watu.
Makamu wa Rais amesema serikali itajenga uwanja wa ndege katika mkoa huo ili kuweza kusafirisha mazao ikiwemo parachichi kwa urahisi. Pia amesema serikali kupitia Latra itashughulikia changamoto ya nauli kuwa juu kwa wananchi wa Wilaya za Makete na Wang’ing’ombe licha ya ujenzi wa barabara za lami za kuunganisha wilaya hizo na makao makuu ya mkoa wa Njombe kukamilika.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais ameweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Lugenge uliopo katika Kijiji cha Lugenge mkoani Njombe unaogharimu shilingi bilioni 8.7. mradi huo umefikia asilimia 82 na utakapokamilika unatarajia kuwahudumia wananchi elfu kumi.
Makamu wa Rais ameagiza mradi huo kukamilika kwa wakati. Aidha amesihi wananchi wa mkoa wa Njombe kutunza vyanzo vya maji na kulinda mazingira ili miradi hiyo maji iwe na manufaa kwao. Amesisitiza kila mmoja kutambua wajibu wa Kupanda miti rafiki wa maji, kuepuka kuchoma moto ovyo na kulinda mazingira.